Raul kushoto |
MSHAMBULIAJI wa Schalke 04, Raul amechangia jezi yake na bao
lake la 400 alilofunga katika kumbukumbu ya soka ya Ujerumani.
Mpachika mabao huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Raul alifunga
bao hilo Februari 19 katika ushindi wa 4-0 kwenye Bundesliga dhidi ya
Wolfsburg.
"Nimekuwa na wakati mzuri sana Bundesliga na ninajivunia
sana heshima niliyopewa na mashabiki wa Ujerumani," alisema Raul, ambaye
amefunga mabao 33 tangu ajiunge na Schalke majira ya joto 2010.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, amefunga mabao 323 akiwa
na Real Madrid, ambako alianzia soka ya kulipwa mwaka 1994, na alitwaa mataji
matatu ya Ligi ya Mabingwa.
Alifunga mengine 44 akiwa na timu ya taifa ya Hispania na 33 akiwa
na Gelsenkirchen.
0 comments:
Post a Comment