RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Joao
Havelange bado yuko hospitali nchini Brazil akisumbuliwa na maradhi
yaliyosababisha virusi fulani kwenye kifundo chake cha mguu wa kulia.
Hospitali ya Samaritano imesema jana, babu huyo mwenye umri
wa miaka 95, Havelange anapumua bila msaada wa mashine, lakini hali yake bado
ipo chini ya uangalizi wa kina.Havelange alilazwa Jumapili, akisumbuliwa na maradhi ya kudhoofu viungo. Bao haijawekwa wazi kama maradhi hayo yamesambaa.
Havelange aliiongoza FIFA kuanzia mwaka 1974 hadi 1998, alipomuachia Seppe Blatter anayeendelea hadi sasa.
Alistaafu kwenye Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki mwaka jana, kwa sababu za kiafya.
0 comments:
Post a Comment