// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAGE: WACHEZAJI WA TANZANIA HAWAJITUMI, HAWANA MALENGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAGE: WACHEZAJI WA TANZANIA HAWAJITUMI, HAWANA MALENGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 20, 2012

    RAGE: WACHEZAJI WA TANZANIA HAWAJITUMI, HAWANA MALENGO

    
    Rage kulia akiwa na kocha wa klabu yake, Mserbia Milovan
    MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage amesema wachezaji wa Tanzania hawaangalii mbali na wanaona Simba na Yanga ndiyo Ulaya yao, na kwa sababu hiyo daima hawatafanikiwa kwa desturi hiyo. Akizungumza leo bongostaz asubuhi, kiungo huyo wa zamani wa Simba SC, alisema kwamba vyombo vya habari vina wajibu wa kusaidia kuelimisha wachezaji wawe na maono ya mbali, kwani kufanya hivyo kutasaidia kuinua soka ya nchi hii.
    Rage alisema wachezaji wa Tanzania ni wavivu wa mazoezi na hawana malengo zaidi ya kufikiria kuchezea Simba na Yanga.
    Alisema hali hiyo ni tofauti na wachezaji wa Magharibi mwa Afrika, ambao wanafanya mazoezi kwa bidii na ndiyo maana wanafanikiwa.
    Rage alisema wachezaji wa Tanzania wanapokuwa mapumzikoni wanafanya starehe tu, wakati wenzao wa Magharibi wanapokuwa kwenye mapumziko huwa wanafanya mazoezi ya kujiweka fiti na ndio maana viwango vyao huwa havishuki.
    Amewashauri wachezaji wa Tanzania kufanya mazoezi kwa bidii ikiwemo gym, kukimbia ufukweni na kadhalika ili waweze kukuza viwango vyao na hatimaye kufuata nyayo za wenzao kwa kucheza Ulaya.
    Akiuzungumzia mchezo wa Jumapili dhidi ya ES Setif ya Algeria katika Kombe la Shirikisho, Rage alisema maandalizi yanaendelea vizuri na wana matumaini ya kushinda.
    Alisema timu imejifua na sasa ina pumzi ya kucheza dakika 90 na zaidi- hivyo amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushuhudia kandanda safi.
    Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Rwanda, ambao ni Hudu Munyemana atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na Felicien Kabanda, Theogene Ndagijimana na Edouard Bahizi na Kamisaa atakuwa Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe.
    Mechi hiyo namba 45 itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wenye uwezo kumeza mashabiki 60,000 itaanza saa 10:00 jioni na marudiano yatakuwa Aprili 6, mwaka huu nchini Algeria.
    Iwapo Simba itafanikiwa kusonga mbele itacheza mechi ya kwanza nyumbani Aprili 29 mwaka huu na mshindi kati ya El Ahly Shandy ya Sudan na Ferroviario de Maputo ya Msumbiji ambapo ya marudiano itachezwa kati ya Mei 11, 12 na 13 mwaka huu.
    Simba ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki kwenye michuano ya Afrika, baada ya wapinzani wao wa jadi, Yanga kutolewa na Zamalek ya Misri katika Ligi ya Mabingwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAGE: WACHEZAJI WA TANZANIA HAWAJITUMI, HAWANA MALENGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top