// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAGE ASHUSHA MAWE MAZITO, SERIKALI YAMKATA MAINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAGE ASHUSHA MAWE MAZITO, SERIKALI YAMKATA MAINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 09, 2012

    RAGE ASHUSHA MAWE MAZITO, SERIKALI YAMKATA MAINI


    Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Rage akitema cheche
    MWENYEKITI  wa klabu ya Simba, Ismail Rage amesema anaandaa hoja kuipeleka kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF  kwa ajili ya kupinga adhabu ya kukatwa Sh 5 milioni baada ya mashabiki wa soka kufanya vurugu na kuvunja viti wakati walipocheza na Kiyovu.
    Rage amesema kitendo hicho cha TFF kuikata Simba fedha ni hujuma na wana mpango wa kususia kuutumia uwanja wa Taifa endapo hawatasikilizwa.
    Kauli ya Rage imekuja baada ya TFF kuwakata Simba sh 5 milioni bila taarifa kwa madai mashabiki wao walifanya vurugu katika pambano la kimataifa kati ya Simba na Kiyovu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Rage alisema kitendo cha TFF kuwakata Simba mapato yao yaliyotokana na mechi ya Ligi Kuu juzi dhidi ya Kagera Sugar ni dalili za kifisadi na hujuma kwani TFF waliwapa barua Simba baada ya kuwakata huku Rage akipinga na kudai haki haikutendeka.
    Rage alisema hivi sasa anaandaa hoja ambayo ataiwakilisha kwenye Mkutano Mkuu wa TFF na endapo haitasikilizwa hoja hiyo ni dhahiri watatusia uwanja wa Taifa katika mechi zao za Ligi Kuu pamoja na zile za kimataifa.
    "Nimeshangaa hivi navyoongea ndio TFF wanatupa barua ya kutukata fedha wakati tayari wameishakata fedha zetu za mapato dhidi ya Kagera Sugar eti kwa madai mashabiki wetu walifanya vurugu tulipocheza na Kiyovu, mimi nasema hiki sio kitendo cha busara na hizi ni dalili za ufisadi na wakiendelea kutukata naweza kuwashtaki kwa sababu kesi ya hivi hauwezi kuipeleka (FIFA), alisema Rage.
    Katika pambano la marudiano kati ya Simba na Kiyovu zilikusanywa jumla ya 208 milioni huku kiasi cha 27 milioni zikikatwa kwa ajili ya ulinzi, ambapo uongozi wa Simba umehoji matumizi ya fedha hizo na kudai TFF inazinyanyasa klabu kwa kutowalipa ipasavyo huku ikiwakata makato makubwa.
    TFF imeikata Simba kiasi hicho cha fedha baada ya Wizara ya Habari ,Vijana , Utamaduni na Michezo kuitaka TFF kulipa gharama za ukarabati wa Uwanja wa Taifa kutokana na vurugu zilizotokea siku ya mechi ya Simba na Kiyovu ya Rwanda.
    Katika mechi hiyo wakati wa mapumziko mashabiki wanaosadikiwa kuwa wa Simba walihama kwenye jukwaa lao na kwenda kwenye jukwaa ambalo mara nyingi hukaa mashabiki wa Yanga na kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu mkubwa viti katika uwanja Uwanja huo.
    Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi,  Mkurugenzi wa Wizara hiyo,  Leonard Thadeo alisema tathmini ya uharibifu inaonyesha kuwa jumla ya viti 152 viliharibiwa na 11 vilivunjwa kabisa.
    Alisema Wizara imesikitishwa na tukio hilo lisilo la kiistarabu na ambalo lingeweza kuleta maafa makubwa kwa wapenzi na mashabiki ambao walihudhuria kwenye mchezo huo, lakini kama haitoshi limeleta fedheha kwa Taifa.
    Thadeo alisema sababu zilizowafanya waibane TFF kulipa gharama hizo na sio Simba ni kwamba wao hawaongei na timu kwani anayekwenda kuomba Uwanja ni TFF na sio timu hivyo hawaoni sababu ya kuongea na mtu au watu ambao hawakuingia nao mkataba wa matumizi ya Uwanja, hilo ni jukumu la TFF kuongea na wadau wao.
    “Kutokana na uharibifu mkubwa uliofanyika, Wizara inaiagiza TFF kulipa kiasi cha shilingi milioni tano (5,000,000) kwa ajili ya matengenezo na urejeshaji wa viti vyote vilivyoharibiwa,”alisema Thadeo.
    Thadeo aliongeza kuwa pamoja na kulipa kiasi hicho cha fedha TFF inatakiwa kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua kali kwa wote watakaobainika kuhusika na vurugu hizo.
    “Iwapo vurugu za namna hiyo zitaendelea Wizara italazimika kufunga kwa muda matumizi ya Uwanja huo,"alisema Thadeo.
    Naye Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura akilizungumzia suala hilo alisema wanazo taarifa hizo za serikali za kutakiwa kulipa gharama za uharibifu huo na watachukua hatua za kinidhamu kwa kila aliyehusika.
    Alisema taarifa kutoka kwa kamisaa wa mchezo huo zinaonyesha kuwa waliohusika na uharibifu huo ni mashabiki wa timu ya Simba ambao walihama kutoka jukwaa ambalo wamezoea kukaa na kwenda kwenye jukwaa la Yanga na kuanzisha vurugu hizo.
     “Taarifa za kutakiwa tulipe tunazo mlipaji moja kwa moja ni Simba ambao wanaonekana kuhusika na vurugu hizo, tutawafahamisha zaidi ni nini wanatakiwa kufanya kutokana na gharama hizo,”alisema Wambura.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAGE ASHUSHA MAWE MAZITO, SERIKALI YAMKATA MAINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top