// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PSV YATIMUA KOCHA GUNDU, COCU ACHUKUA MIKOBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PSV YATIMUA KOCHA GUNDU, COCU ACHUKUA MIKOBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 12, 2012

    PSV YATIMUA KOCHA GUNDU, COCU ACHUKUA MIKOBA

    Phillip Cocu
    KLABU ya PSV Eindhoven imemfukuza kocha Fred Rutten leo, kufuatia matokeo mabaya yaliyopunguza matumaini ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Uholanzi msimu huu.
    Nafukuzwa baada ya timu hiyo kupigwa mabao 3-1 Jumapili na NAC Breda, kipigo kinachofuatia kipigo kingine cha 4-2 kwenye Europa League kutoka kwa Valencia ya Hispania na kipigo cha 6-2 kutoka kwa wapinzani wao kwenye mbio za taji, FC Twente.
    Pamoja na kipigo, PSV inabaki nafasi ya nne kwenye ligi ya Uholanzi, Eredivisie, ikizidiwa pointi na vinara, AZ Alkmaar.
    Klabu imesema kiungo wa zamani wa Uholanzi, Phillip Cocu na beki wa zamani wa PSV, Ernest Faber wwatakuwa makocha wa muda wa klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
    Cocu amekuwa Msaidizi wa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Bert van Marwijk tangu 2008.
    Ameichezea nchi yake mechi 101 na pia aliichezea PSV kuanzia 1995 hadi 1998 kabla ya kutimkia Barcelona hadi 2004. Baadate alirejea PSV ambako aliisaidia klabu hiyo kutwaa mataji matatu mfululizo ya ligi kuanzia msimu wa 2005-07.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PSV YATIMUA KOCHA GUNDU, COCU ACHUKUA MIKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top