// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MABADILIKO MISS TANZANIA/WORLD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MABADILIKO MISS TANZANIA/WORLD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 15, 2012

    MABADILIKO MISS TANZANIA/WORLD




    PRESS RELEASE
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    15  MACHI 2012

     MABADILIKO YA KALENDA YA  MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA:

     Katika mkutano wa mawakala wa wanaoandaa mashindano ya urembo kutoka nchi mbalimbali duniani uliofanyika London Uingereza mwezi Novemba 2011, Tulijulishwa mabadiliko ya Kalenda ya mashindano ya urembo ya dunia.  [Miss World.]

    Mashindano ya urembo ya Dunia yanatarajia kufanyika mwezi August 2012 nchini China, badala ya mwezi Novemba/ Desemba kama ilivyozoeleka, ambapo washiriki kutoka nchi mbalimbali watatakiwa wawe wamefika nchini China mwezi Julai 2012. 
    Kutokana na hali hiyo tunalazimika kubadilisha kalenda ya mashindano yetu kama ifuatavyo:- 
    1. Tutatuma Mwakilishi atakayeshiriki mashindano ya urembo ya Dunia Miss World 2012. 
    2. Mwakilishi  huyo atapatikana kwa njia ya usaili.  Ambapo warembo watakaojitokeza katika usaili huo  watafanyiwa  mchujo na kupatikana   idadi ya warembo 10  watakaopanda jukwaani katika tafrija ndogo ili kumpata Mwakilishi  ambaye atabeba Bendera ya Tanzania katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia   2012. 
    3. Tunaomba warembo wote wenye sifa na nia ya kushiriki  katika mchujo wa usaili  wawasiliane na ofisi zetu au Mawakala wete popote Tanzania kupata maelezo zaidi.

     Mchakato wa mashindano ya Redds Miss Tanzania 2012 katika ngazi zote utaendelea kama kawaida  na Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2012 atawakilisha nchi yetu katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, akiwa na muda wa miezi [7] saba ya maandalizi.

    Hii inakidhi haja na maoni ya Wadau wa fani ya urembo ya kumpa muda wa kutosha Mrembo wa Taifa kujiandaa vya kutosha kabla ya kushiriki Fainali za dunia.

    Lundenga
     HASHIM LUNDENGA.
     MKURUGENZI. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABADILIKO MISS TANZANIA/WORLD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top