Messi |
Hiyo inafuatia, vinara hao wa La Liga, Real Madrid kulazimishwa sare Jumatano.
Messi alivunja rekodi ya upachikaji mabao Barcelona na kuwasaidia mabingwa hao watetezi, kupunguza idadi ya pointi wanazozidiwa na Real Madrid kutoka 10 hadi sita.
Lakini baadaye leo, Madrid nayo itakuwa mwenyeji wa Real Sociedad wakihitaji ushindi ili kurudisha matumaini mapema.
Madrid itacheza bila kocha wake Jose Mourinho, beki Sergio Ramos na kiungo Mesut Oezil, wanaotumikia adhabu ya mechi moja moja baada ya kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu waliouonyesha kwenye mechi iliyopita, wakitoka sare ya 1-1 na Villarreal Jumatano.
Pepe amefungiwa pia, mechi mbili baada ya kukutwa na hatia ya kumtukana refa siku hiyo kwenye Uwanja wa El Madrigal.
Hivyo mechi ya leo itawafanya Madrid wawakose mabeki wake wote wa kati na mmoja kati ya washambuliaji wake hatari na wingta Angel Di Maria, ambaye ni majeruhi.
Pamoja na sare mbili mfululizo, beki wa Real, Marcelo alisema Madrid bado wana nafasi ya kutwaa taji la lao la kwanza la La Liga ndani ya miaka minne.
"Nafikiri kwamba timu yoyote ingependa kuongoza kwa pointi sita," alisema Marcelo. "Tunatakiwa kutulia. Hatukushinda, lakini morali ya timu iko juu."
Sociedad imefungwa mechi nne zilizopita nje ya Uwanja wa Anoeta.
Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola atatakiwa kuunda safu nyingine ya ulinzi, kufuatia Dani Alves kuwa anatumikia adhabu, Adriano majeruhi na Eric Abidal anasubiri kufanyiwa upasuaji wa ini.
Waburuza mkia Zaragoza watakuwa wenyeji wa Atletico Madrid Jumapili wakitarajia kuendeleza wimbi la ushindi, baada ya kuichinja 2-1 Valencia Jumatano, wakitokea nyuma, shukrani kwake Antonio "Apono" Galdeano aliyefunga mabao mawililicha ya timu yake kucheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa takriban nusu saa.
Mechi nyingine Jumapili ni: Espanyol v Malaga, Rayo Vallecano v Villarreal na Real Betis v Racing Santander. Valencia wanaoshika nafasi ya tatu wataifuata Getafe leo na Granada watakuwa wenyeji wa Sevilla kesho.
0 comments:
Post a Comment