// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAMBANO KALI MAKKA YA NDONDI USIKU WA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAMBANO KALI MAKKA YA NDONDI USIKU WA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 17, 2012

    PAMBANO KALI MAKKA YA NDONDI USIKU WA LEO


    Sergio Martinez 
    BONDIA Sergio Martinez kwa ujumla anachukuliwa kama bondia bora wa uzito wa Middle, licha ya jkwamba hana taji lolote kubwa. Anaweza kuanza vema kupiga hatua kuelekea huko, katika pambano lake la leo kwenye ukumbi wa Madison Square Garden dhidi ya Matthew Macklin, mzaliwa wa England kutioka kwa wazazi wa Ireland.
    Muargentina huyo mwenyr umri wa miaka 37, rekodi yake ni 48-2-2, akiwa ameshinda mapambano yake manne yaliyopita na leo anapigana kwa mara ya kwanza Garden.
    “Imekuwa ndoto yangu katika maisha yote kupigana makka ya ngumi, Madison Square Garden,” alisema Martinez. “Nimekuwa nikifikiria kupigana hapa kwa miaka mingi.”
    Dogo wa miaka 29, Macklin rekodi yake ni 28-3 na anaingia kwenye pambano hilo akitoka kupigwa kwa utata na bingwa wa WBA, Felix Sturm nyumbani kwa mpinzani wake huyo, Ujerumani.
    Anashikilia mataji ya England, Uingereza, Ireland na Ulaya na sasa anapigania taji la dunia.
    “Hii ni kwa ajili ya nafasi ya kwanza katika uzito wa Middle,” alisema Macklin, ambaye jina lake la utani ni Mack The Knife. “Leo ni miaka 18 tangu nipande ulingoni kwa mara ya kwanza, Birmingham, England. Wakati wote niliamini nitakuwa bingwa wa dunuia.”
    Pambano la utangulizi litakutanisha mabondia mawili wenye majina ya utani yanayofanana na staili zao za kupigana. Edwin “La Bomba” Rodriguez ambaye hajawahi kupigwata atazipiga na Donovan “Da Bomb” George.
    Rodriguez amepiga Knockout 14 katika mapambano yake 20 aliyoshinda, wakati George ana Knockout 19 katika rekodi yake ya 22-1-1.
    “Niko tayari kutuma ujumbe kwa mabondia wote vigogo wa uzito wa Super Middle duniani, kwamba nipo pembeno yao,” alisema Rodriguez.
    Martinez-Macklin ni kwa ajili ya taji la dhahabu la WBC, usilichanganye na taji la ubingwa la WBC ambalo Martinez alilitwaa 2010. Alilazimishwa kuachia taji kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, lakini bado anaheshimiwa kama bingwa wa Middle.
    “Sergio ni bingwa halisi wa Middle,” alisema Macklin, “Na kama unataka kuwa bora lazima uwapige walio bora. Nafurahi kupata nafasi hiyo.
    “Ana miaka 37 sasa na Jumamosi usiku, atapitia kila siku katika miaka yake 37. Na huko nitakuwa bingwa mpya wa dunia wa Middle.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBANO KALI MAKKA YA NDONDI USIKU WA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top