// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PACQUIAO AKABILIWA NA TUHUMA ZA UFISADI, JELA YAMUITA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PACQUIAO AKABILIWA NA TUHUMA ZA UFISADI, JELA YAMUITA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2012

    PACQUIAO AKABILIWA NA TUHUMA ZA UFISADI, JELA YAMUITA


    Manny Pacquiao kulia akipigana na Mmarekani Shane Mosley Mei 7, mwaka jana.


    MAOFISA Kodi wa Philippine, wamemfungulia malalamiko ya uhalifu bingwa wa ndondi na Mbunge ambaye anahusika katika kutunga sheria, Manny Pacquiao kwa kushindwa kuwasilisha makabrasha uili kufanyiwa uchunguzi ulipaji wake wa kodi.
    Waendesha mashitaka wataamua kama kuna ushahidi wa kutosha ili kupeleka suaal hilo mahakamani, ambako Pacquiao anaweza kutupwa jela kwa miaka miwili iwapo atakuwa na hatia.
    Mkurugenzi wa Idara ya Mapato ya Ndani, Rozil Lozares amesema kwamba malalamiko yalifunguliwa Machi 1, baada ya Pacquiao kushindwa kuwasilisha makabrasha licha ya kupelekewa taarifa mara tatu.
    Alisema juzi kwamba taarifa za kodi za Pacquiao mwaka 2010 zina utata na ndizo waataka kuzifanyia uchunguzi, lakini yeye anakwepa.
    Pacquiao ambaye jarida la Forbes Magazine mwaka jana lilimtaja kama mwanamichezo anayeshika nafasi ya 24 duniani kwa utajiri, alipopigiwa simu ili kujibu tuhuma hizo, ilikuwa inaita bila majibu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PACQUIAO AKABILIWA NA TUHUMA ZA UFISADI, JELA YAMUITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top