Ozile |
KIUNGO wa Real Madrid, Mesut Ozil amesema alikuwa ana nafasi
ya kujiunga na Inter Milan baada ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010, lakini
akaamua kwenda Santiago Bernabeu.
Sasa mambo yakiwa yamemnyookea Hispania, amesema anapenda
kucheza Los Blancos hadi anastaafu.
Gazeti la Sport-Bild limeripoti kuwa kocha wa zamani wa
Inter Milan, Jose Mourinho kwanza alitaka kumsajili Ozil ahamie Serie A mwaka
2009, lakini akachelewa kuwahi dirisha la usajili.
The Nerazzurri tena wakajaribu kumsajili mshambuliaji huyo
wa zamani wa Werder Bremen kwa dau la Euro Milioni 25 kuimarisha safu ya kiungo
katika kushambulia, lakini bahati mbaya
Ozil akili yake ilikuwa kuhamia Madrid, alikohamia kwa dau la
Euro Milioni 15 kuungana na Mourinho.
"Ni kweli kwamba 2010 nilipata ofa kutoka klabu kibao
kubwa Ulaya. Ikiwemo Inter. Lakini uamuzi wa kwenda Real ulikuwa sahihi.
Ni klabu bora duniani, na ningependa kumalizia soka yangu
hapa," alisema Ozil.
"Nina miaka 23 tu, sitakuwa kwenye kiwango cha juu kwa
muda mrefu. Hata niwe bora aje. Akili yangu yote ni Madrid na timu ya taifa,
kwa sababu tunaweza kuweka historia mwaka huu.
"Sisi [Real] tunaweza kutwaa La Liga na Ligi ya
Mabingwa, na Euro nikiwa na Ujerumani."
Nyota huyo wa Madrid alizungumzia pia kiwango cha
mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi na hakuwa na cha zaidi ispokuwa kumtukuza
Muargentina huyo.
0 comments:
Post a Comment