Senegal na Morocco |
SIMBA wa Teranga, Senegal watamenyana na Oman katika mechi
maalum ya kuwania tiketi ya kucheza Olimpiki mwaka huu, London, mchezo
utakaofanyika Aprili 23 mjini Coventry.
Mechi hiyo itaamua timu ya mwisho yab kukamilisha idadi ya
timu 16 za kucheza Olimpiki inayotarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka
huu.
Simba wa Teranga wamepata nafasi hiyo baada ya kushika
nafasi ya nne katika michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 23 iliyofanyika
Morocco Desemba mwaka jana.
Oman inayofundishwa na Mfaransa, Paul Le Guen walipata
nafasi hiyo baada ya kuifunga Uzbekistan 2-0 Alhamisi katika mechi ya mwisho ya
kuwania kufuzu kucheza fainali hizo kwa bara la Asia.
Gabon, Morocco Misri ni wawakilishi wengine wa Afrika kwenye
Olimpiki ya mwaka huu.
Timu nyingine zilizofuzu ni mbali na wenyeji Uingereza, ni Korea
Kusini, Japan, Falme za Kiarabu kwa Asia (AFC); Brazil na Uruguay kwa Amerika
Kusini (CONMEBOL); Uswisi, Hispania na Belarus kwa Ulaya (UEFA) na New Zealand
(OCEANIA).
Wawakilishi wengine wawili watoka Amerika Kaskazini, CONCACAF
ambao michuano yao inatarajiwa kumalizika Jumatatu ijayo.
0 comments:
Post a Comment