// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NYOTA YANGA AWABEBA SOFAPAKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NYOTA YANGA AWABEBA SOFAPAKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 06, 2012

    NYOTA YANGA AWABEBA SOFAPAKA


    KLABU ya Sofapaka imeifunga Rangers mabao 2-1 katika mechi kali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo jana.
    Sofapaka ilipata bao la kwanza dakika ya 10, wakati Abdallah Juma alipofunga kwa mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 30, ambao ulimshinda kipa wa Rangers, Victor Omondi na bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
    Rangers ilisawazisha dakika ya 57, wakati Michael Ochieng alipofunga bonge la bao baada ya kuwatoka mabeki wawili kabla ya kumtungua kipa wa Sofapaka, Duncan Ochieng.
    Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, John Barasa aliifungia Sofapaka bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Rangers kumkwatua kwenye boksi Robert Binja aliyetokea benchi na refa akaamuru adhabu hiyo, iliyotumiwa vyema na mkongwe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA YANGA AWABEBA SOFAPAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top