// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
NIZAR KHALFAN ATEMWA PHILADELPHIA UNION MIEZI MITATU TANGU ASAJILIWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINENIZAR KHALFAN ATEMWA PHILADELPHIA UNION MIEZI MITATU TANGU ASAJILIWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
NIZAR KHALFAN ATEMWA PHILADELPHIA UNION MIEZI MITATU TANGU ASAJILIWE
Nizar akishangilia moja ya mabao yake Vancouver
Nizar mazoezini na Philadelhphia Union
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan ametemwa na
klabu ya Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya Marekani na sasa hana timu.Habari za uhakika kutoka Marekani, ambazo bongostaz imezipata
zimesema kwamba, Nizar ambaye wiki iliyopita alionekana Dar es Salaam, alitemwa
na klabu hiyo miezi mitatu tu tangu achukuliwe baada ya kufuzu majaribio.Nizar alikwenda kufanya majaribio Union, baada ya kutemwa na Vancouver,
Novemba 23, mwaka jana.Nizar aliyezaliwa Juni 21, mwaka 1988 mjini Mtwara, alijiunga
na Vancouver Whitecaps FC ya Canada Agosti 22, mwaka 2009 akitokea Moro United
ya Ligi Kuu ya Bara na akacheza mechi tisa msimu wa kwanza wa 2009 na
kuongezewa mkataba wa kuichezea timu hiyo msimu uliofuata wa 2010.Alifunga bao lake la kwanza Whitecaps Juni 12, mwaka 2010 katika
mechi dhidi ya Austin Aztex na haikushangaza Februari 9, mwaka jana aliposaini
mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya timu hiyo kupanda Ligi Kuu ya Marekani,
maarufu kama Major League Soccer.Hata hivyo, baada ya msimu huo timu yake ikirejea Daraja la
kwanza, Niazar akatemwa na kwenda Philadelphia Union, ambako miezi mitatu
baadaye ametemwa nako.Juhudi za kumpata Nizar kuzungumzia mustakabali wake zinaendelea.Kabla ya Moro United, Nizar aliyeibukia kwenye timu ya taifa
ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004, alichezea Mtibwa Sugar FC, na baadaye akanunuliwa na Al Tadamon ya Ligi
Kuu ya Kuwait msimu wa 2007-2008.Januari 2008 aliondoka Al Tadamon na kusaini mkataba na Tadamon
Sour ya Lebanon, ambako alipomaliza mkataba wake akarejea Tanzania kuchezea
Moro United.
Afcon Preview: Nigeria host Rwanda
-
Having sealed their Africa Cup of Nations involvement, Nigeria host
Rwanda in Monday’s final qualifying game at Godswill Akpabio Stadium,
aiming to en...
Lotte and Leah comment on derby win
-
Lotte Wubben-Moy and Leah Williamson share their post-match thoughts
following our 3-0 win away to Tottenham Hotspur Women
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment