// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NEYMAR ATUPIA TATU MTANANGE WA WATANI WA JADI BRAZIL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NEYMAR ATUPIA TATU MTANANGE WA WATANI WA JADI BRAZIL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 08, 2012

    NEYMAR ATUPIA TATU MTANANGE WA WATANI WA JADI BRAZIL


    Neymar

    KINDA la Kibrazil, Neymar limepiga mabao matatu peke yake wakati Santos ikiitandika Internacional 3-1 katika mechi ya wapinzani wa jadi Brazil, hatua ya makundi ya Copa Libertadores usiku wa jana, wakati Fluminese iliichapa Boca Juniors 2-1 na kuvunja rekodi ya klabu hiyo ya Argentina kutofungwa kwenye mechi 36 katika mashindano yote.
    Hat-trick ya Neymar inawapa mabingwa watetezi, Santos ushidni wa kwanza katika mashindano hayo mwaka huu na kuipeleka klabu hiyo katika nafasi ya pili kwenye Kundi la 1 kwa pointi zake tatu kwenye mechi mbili.
    Katika Kundi la 4 mjini Buenos Aires, kiungo wa zamani wa Chelsea na Ureno, Deco alimtengenezea bao la kwanza Fred aliloifungia Fluminese dakika ya 10 na kufunga la ushindi dakika ya 55, baada ya Leandro Somoza kuisawazishia Boca dakika mbili baada ya mapumziko.
    Matokeo hayo yanaifanya Fluminense kufikisha pointi sita kwenye Kundi la 4, wakati Boca ina pointi moja tu katika nafasi ya tatu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NEYMAR ATUPIA TATU MTANANGE WA WATANI WA JADI BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top