|
Mwenyekiti wa KRFA kulia |
SIKU mbili baada ya kuchaguliwa kwa Jamal Malinzi kuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Bukoba (KRFA), chama hicho kimetangaza nafasi ya
kazi kwa Ofisa Tawala, ambaye wajibu wake utakuwa ni kusimamia shughuli za kila
siku za chama.
Akizungumza na bongostaz mchana huu, Mwenyekiti mpya wa
KRFA, Malinzi alisema kwamba mwombaji anatakiwa na umri kati ya miaka 25 hadi
40 na awe na elimu ya kuanzia kiwango cha Stashahada, ingawa wenye Shahada
atapewa kipaumbele.
Alisema mwombaji anatakiwa kujua kituo chake cha kazi kitakuwa
Bukoba na atawajibika chini ya Katibu Mkuu.
KRFA kinakuwa chama cha kwanza cha soka cha mkoa kuajiri
Ofisa Tawala katika historia ya soka ya nchi hii, jambo ambalo linaashiria
chama hicho chini ya Malinzi kimepania kuleta mageuzi katika soka ya mkoa huo.
0 comments:
Post a Comment