Messi, ataendeleza cheche zake leo? |
HARAKATI za AC Milan kuwadondosha mabingwa wa Ulaya ni kama
zimeingia doa kwa beki wake wa kati, Thiago Silva, ambaye alifunga bao katika
sare ya 2-2 timu hizo zilipokutana msimu huu, kuumia katika mechi na AS Roma.
Atazikosa mechi zote za Robo Fainali, inamaanisha kocha
Massimiliano Allegri ataisuka upya safu yake ya ulinzi, akimrejesha beki
mkongwe, Alessandro Nesta. Daniele Bonera atateleza beki ya kulia kuchukua
nafasi ya majeruhi Ignazio Abate.Mchezaji mwingine tegemeo ambaye atakosekana ni kiungo Mark Van Bommel anayetumikia adhabu, kakini Kevin-Prince Boateng na kiungo mchezeshaji Clarence Seedorf kwa mara nyinginer tena watakuwepo na wote wanaweza kuanza, ingawa Alberto Aquilani na Urby Emanuelson pia wanatarajiwa kuanza.
Ibrahimovic, ambaye anaongoza kwa mabao Serie A akiwa amefunga 22, ataongoza safu ya ushambuliaji. Robinho amepona maumivu ya kifundo cha mguu na anatarajiwa kuanza sambamba na nyota wa zamani wa Inter, Maxi Lopez na Stephan El Shaarawy.
Alexandre Pato amekwenda Marekani kwa tiba, kutokana na matatizo ya misuli na hatacheza leo.
Barcelona kwa sasa ina hofu chache wakati beki wake Eric Abidal akienda kufanyiwa upasuaji wa ini, beki mwingine, Adriano ni mgonjwa.
Pamoja na hayo, Carles Puyol anaweza kwenda kucheza beki ya kushoto na Javier Mascherano akasimama na Gerard Pique katika beki ya kati.
Kocha Pep Guardiola anaweza kutumia mfumo wa 3-4-3 ambao aliutumia dhidi ya AC Milan mapema katika hatua ya makundi.
Winga Mholanzi, Ibrahim Afellay amehusishwa kwenye kikosi cha leo na anaendelea na mazoezi, lakini hatacheza, kufuatia kupona kwake goti. Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, David Villa bado ni majeruhi wa muda mrefu.
Nani atacheza sambamba na Lionel Messi pale mbele, bado inabakiwa kuwa siri, lakini watu wenye kasi mbele wanaweza kuwa Cesc Fabregas na Alexis Sanchez na Pedro huwezi kumuacha kumfikiria kwenye 11 wa kuanza.
VIKOSI VYA
LEO:
AC MILAN: Abbiati, Bonera, Nesta, Mexes, Antonini, Aquilani,
Ambrosini, Nocerino, Boateng, Ibrahimovic na Robinho.BARCELONA: Valdes, Dani Alves, Mascherano, Pique, Puyol, Xavi, Busquets, Iniesta, Cesc, Messi na Sanchez.
JE WAJUA?
•AC Milan haijawhai kufungwa mechi ya nyumbani katika Robo
Fainali ya michuano hiyo ya Ulaya, imeshinda 10 na kutoa sare nne.
•Mabingwa hao wa Serie
A wamefungwa mabao 11, ambayo ni mengi kwa timu zote zilizofika hatua hii msimu
huu.
•Wacheazaji wa sasa wa
Milan Ibrahimovic, Maxi Lopez, Van Bommel na Zambrotta wamepitia The Blaugrana katika
historia zao.
•Barcelona tayari
imeifunga AC Milan Uwanja wa San Siro msimu huu, ikishinda 3-2 katika mechi ya Kundi H.
•Kikosi cha Guardiola
kiliongoza Kundi H kwa pointi zake 16 na Wataliano walikuwa wa pili kwa pointi
zao tisa.
•The Catalans wameshinda
mechi tisa mfululizo kwenye mashindano yote tangu wafungwe 3-2 na Osasuna mapema
Februari.
0 comments:
Post a Comment