Muamba |
Muamba alikuwa anakimbia mpira katika mechi ya Kombe la FA Machi 17, 2012 kabla ya kuanguka na kuzimia uwanjani.
Lakini mzaliwa huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameonyesha kuimarika kiafya jana na kufika jioni hakuwa kwenye hali mbaya tena.
Rafiki wa Muamba, Curtis Codrington, alisema family ya mchezaji huyo ilimuambia kwamba jamaa ameanza kuzungumza kidogo kidogo maneno ya Kiingereza na Kifaransa, ambayo ni nafuu kuliko kuwa kimya kabisa.
Hayo yalithibitishwa baadaye na kiungo wa Chelsea, Michael Essien baada ya kumtembelea kiungo mwenzake huyo hospitali.
Mpenzi wa mchezaji huyo aliwashukuru madaktari na pia wachezaji wenzake walio bega kwa began aye katika wakati huu mgumu.
“Wachezaji wote wanahangaika, nawashukuru sana,” alisema Shauna Muamba.
Wapenzi hao wana motto wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, Joshua na walivishana pete ya uchumba katika Valentine’s Day.
Muamba, mchezaji wa zamano wa Arsenal na Birmingham, alihamia England na familia yake mwaka 1999 kukimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe Kongo.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter pia amemuandikia Mwenyekiti wa Bolton, Phil Gartside jana akimtakia heri Muamba.
Mechi ya leo ya Bolton na Aston Villa katika Ligi Kuu ya England imeahirishwa na timu hiyo sasa itacheza na Blackburn Jumamosi na wanaweza kucheaza tena na Tottenham wiki ijayo kwenye Uwanja wa White Hart Lane yakiwa marudio ya mechi yao ya Kombe la FA iliyovunjika Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment