// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MTOTO WA WHITNEY AFUNGUKA, ASEMA MAMA YAKE HUWA ANAMTOKEA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MTOTO WA WHITNEY AFUNGUKA, ASEMA MAMA YAKE HUWA ANAMTOKEA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 12, 2012

    MTOTO WA WHITNEY AFUNGUKA, ASEMA MAMA YAKE HUWA ANAMTOKEA

    MTOTO pekee wa marehemu wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown, amevunja ukimya na kufunguka, akisema mama yake humtokea na kuzungumza naye.
    Bobbi alisema kwamba siku yote ya mwisho ya uhai wa mama yake alikuwa amejilaza kwenye mkono wake. Binti huyo mwenye umri wa miaka 19 alimuambia Oprah Winfrey katika shoo ya Oprah's Next Chapter, hiyo ikiwa ni interview yake ya kwanza tangu kufariki kwa Houston, aliyekutwa amekufa katika chumba cha hoteli yake Februari 11, mwaka huu.
    Usiku wa kuamkia kifo cha Houston, binti yake huyo, mtoto wa mume wake wa zamani, mwimbaji Bobby Brown alimuomba mama yake kulala naye kama ilivyokuwa kawaida yao.
    “Wakati fulani alikuwa anakuja chumbani kwangu, analala na mimi,” alisema Bobbi Kristina kumuambia Winfrey. “Katika siku ya mwisho, ilikuwa mapema sana. Nilienda kumchukua. Nilisema, “Mama, utakuja kulala na mimi?” alikaa na mimi siku nzima. Nililala katika mkono wake siku yote. Usiku wote mrefu.”
    Bobbi Kristina ametokea kuwa mwenye kujiamini na jasiri kuliko unavyoweza kumfikiria mtoto wa umri kama wake aliyefiwa na mama yake. Bobbi Kristina alizungumza na Winfrey katika nyumba yake ya Atlanta, anapoishi na mjomba na shangazi yake. Kaka yake Houston, Gary na mkewe, Patricia, ambaye alikuwa Meneja wa Houston.
    Bobbi Kristina alisema sapoti anayopata kutoka kwa familia yake na Mungu inatosha kumsaidia kumpoza machungu ya kumpoteza mama yake kipenzi. Pia anatokewa na mama yake, ambaye alisema bado anazungumza naye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTOTO WA WHITNEY AFUNGUKA, ASEMA MAMA YAKE HUWA ANAMTOKEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top