Bert Sugar |
GWIJI wa uandishi na uchambuzi wa habari za ngumi, Bert
Sugar, ambaye ni maarufu kwa vazi lake la kofia ya pama na kuvuta cigar, amefariki
jana Jumapili akiwa ana umri wa miaka 75.
Mtoto wake wa kike, Jennifer Frawley, na mke wake, Suzanne, walikuwa pamoja naye
wakati anakata roho katika hospitali ya Northern Westchester. Sugar alikuwa anasumbuliwa na saratani kwa muda mrefu.
Sugar aliingizwa katika orodha ya watu wenye mchango mkubwa kimataifa daima katika mchezo wa ngumi mwaka 2005, akiwa ameandika zaidi ya vitabu 80, kikiwemo “The 100 Greatest Boxers Of All Time.
Pia ameshiriki filamu kadhaa za ndondi ikiwemo “The Great White Hype”, ambayo starring wake ni Samuel Jackson.
“Bila Bert, mambo yatabadilika sana pembezoni mwa ulingo,”alisema Jack Hirsch, rais wa Chama cha Waandishi wa Habari za Ngumi Marekani.
Sugar alizaliwa Washington, D.C., mwaka 1936 na alihitimu masomo yake Maryland na kwenda kusomea sheria Michigan.
Kabla ya kuanza kuandika ndondi, alifanya kazi ya matangazo nyumbani kwao New York City miaka ya 1970.
Frawley alisema matayarisho ya mazishi yake yanaendelea na yeyote anayetaka kutoa mchango wake kwenye msiba huo, apitie Boxing Hall Of Fame.
0 comments:
Post a Comment