Marafiki wa mashaka, Mourinho kulia na Casilas kushoto |
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho ameamua kumuuza kipa
Iker Casillas mwishoni mwa msimu kuliko kujaribu kuboresha uhusiano wao.
Katika siku za karibuni, kumekuwa kuna tetesi kwamba
Mourinho anaweza kumuuza Casillas kutokana na kuzidi kutitia katika bifu.Habari za ndani zaidi zinasema kwamba, Kocha huyo Mreno kumuuza Casillas, ambaye amekuwa kipa namba moja wa Real Madrid kwa zaidi ya muongo mmoja, litakuwa jambo gumu.
Ni kwamba, viongozi wa klabu hiyo wamekubaliana kwa siri ni bora kumpoteza Mourinho kuliko Casillas.
Ni wazi kwamba Mourinho anamuona Casillas kama tatizo. Amekuwa akisema kipa huyo anajiona babu kubwa tangu atwae Kombe la Dunia, mwaka juzi akiwa na Hispania.
Katika kuonyesha kwamba kipa huyo si chochote kwake, baada ya mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 30 kudaka vema dhidi ya Lyon, Mourinho aliseme kwa dharau:
"Ameokoa michomo fulani vizuri kama kipa yoyote anavyoweza kufanya katika timu muhimu. Ndicho anatakiwa kufanya."
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Nahodha huyo wa Real Madrid, mara zote amekuwa hakubaliano na Mourinho kwa sheria na mipango yake kwamba haiendani na wao.
Casillas yuko poa tu kutofautiana na kocha wake, akiwa ameiichezea klabu hiyo kwa miaka mingi.
Msimu huu, tetesi zimeibuka kwamba Mourinho aliulizia kuondoka kwa Casillas kutokana na ugomvi baina yao.
Casillas alimpigia simu mchezaji wa Barcelona kuelekea katika mechi ya Supercopa baina ya timu hizo Agosti, mwaka jana kitu amabcho kilimkera Mourinho, aliyezuia mawasiliano na wachezaji wa wapinzani wao na anampiga chini kwenye mechi na Galatasaray.
Baadaye, Mourinho aliandaa pati maalum ya kukutana ili kumaliza tofauti zake na wachezaji wake, ambao walionekana kuongozwa na Casillas leader.
Hivi karibuni, ulitokea mtafaruku baina ya Sergio Ramos na Mourinho ambao ulikuzwa kwenye vyombo vya habari Hispania, na Casillas akionekana kama kiini.
Kocha huyo, alitaka kumvua Unahodha, ingawa akaachana naye.
Lakini upande wa pili, mashabiki wanamkubali zaidi Mourinho kuliko Casillas, hasa baada ya kufanya madudu kwenye mechi dhidi ya Malaga na Villarreal.
Wakati huo huo, habari zinasema kwamba Los Blancos wanasaka kipa. Wapo kwenye mazungumzo na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer, sambamba na Thibaut Courtois, ambaye yupo kwa mkopo Atletico Madrid kutoka Chelsea. Lakini ukweli ni kwamba kipa mpya akija atafikia benchi.
0 comments:
Post a Comment