WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wamejiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye
michuano ya Kombe la Shiriksiho la Soka Afrika baada ya kuifunga ES Setif ya
Algeria katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya michuano hiyo.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo mshambuliaji wa
kimataifa wa Uganda, Emanuel Arnold Okwi na Mzambia Felix Mumba Sunzu Jr.
waliofunga mabao hayo kipindi cha pili.Setif waliocheza mchezo wa kujihami zaidi kabla ya kufungwa, waliwabana Simba vema na kufanikiwa kutoka nao suluhu ya bila kufungana baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Lakini baada ya kupokea mawaidha ya kocha wao Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick, Wekundu wa Msimbazi walibadilika kipindi cha pili kwa kuongeza kasi ya mashambulizi na hatimaye kupata mabao mawili ndani ya dakika tatu.
Okwi alianza dakika ya 79 kwa kufunga bao zuri kwa shuti la chinichini- na baada ya bao hilo wachezaji wa Setif walionekana kubadilisha mchezo na kuanza kupanda kushambulia kwa kasi na nguvu kwenye lango la Simba.
Simba walitumia mwanya huo kufanya shambulizi la kushitukiza na mchezaji mmoja wa Setif akamuangusha Okwi kushoto mwa Uwanja na Salum Machaku Salum akaenda kupiga mpira wa adhabu ambao uliunganishwa nyavuni na Sunzu dakika ya 80.
Simba ilichangamka zaidi baada ya bao hilo na kutengeneza nafasi nyingine kadhaa za kuongeza mabao, lakini ama Setif waliokoa au Simba wenyewe walipoteza.
Kwa matokeo hayo, Simba sasa inahitaji hata sare katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye kwenye Uwanja wa nyasi bandia uitwao Mei 8, mjini Stif uliofunguliwa mwaka 1972 na kukarabatiwa mwaka 2008, ukiwa na uwezo wa kumeza watu 25,000 tu.
Setif inakuwa timu ya tatu kihistoria kumenyana na Simba SC, baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kutolewa na JET katika Klabu Bingwa Afrika, kabla ba wao kuitoa Al harrach katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa ujumla Simba ni mabalozi wazuri wa Tanzania katika michuano ya Afrika na wamekuwa wakifanya vema kila wanapomenyana na timu kutoka Kaskazini mwa Afrika.
LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
MWAKA 1974:NUSU FAINALI:
Simba Vs Mehallal 1-0: 0-1
(Mehalla ilishinda kwa penalti 3-0, ingawa kuna habari za kipa wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu) kufanyiwa fujo, wakati wa upigwaji wa penalti.
MWAKA 1981:
RAUNDI YA PILI:Simba ilitolewa na JET ya Algeria.
MWAKA 2003:
RAUNDI YA PILI:
Simba (Dsm) Vs Zamalek 1-0
Zamalek (Misri) Vs Simba 1-0
(Simba ilifuzu kwa penaliti 3-2)
MECHI ZA KUNDI A:
Sept. 7/2003:
Simba Vs Ismaili 0-0Sept. 19/2003: Ismaili (Msri) Vs Simba 2-1
KOMBE LA WASHINDI
MWAKA 1985
RAUNDI YA PILI
Simba SC Vs Al Ahly (Misri) 2-1 0-2
MWAKA 1996
RAUNDI YA PILI
Simba Vs Al Mokaoulun (Misri) 3-1 0-2 3-3 (Al Mokaoulun walifuzu kwa faida ya bao la ugenini)
MWAKA 2001
RAUNDI YA PILIIsmailia (Misri) Vs Simba SC 2-0, 0-1, 2-1
(Mechi ya marudiano ilichezwa mara mbili, baada ya mechi ya kwanza kuvunjika dakika ya 46, SImba ikiwa inaongoza mabao 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam(sasa Uhuru). Ismailia walilalamikia hali ya Uwanja kujaa maji kwamba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo, hivyo kugoma kucheza katika mazingira yale na mchezo ukasogezwa mbele kwa siku moja na ndipo wenyeji waliposhinda 1-0. Hivyo Simba kwa kufungwa 2-0 awali mjini Cairo, walijikuta wakitolewa kwa matokeo ya jumla ya kufungwa 2-1.
Mchezo wa kwanza ulitawaliwa na vurugu, Polisi walivamia uwanjani kuwatawanya wachezaji wa Ismailia kwa mabomu ya machozi, waliokuwa wakimzonga refa kwa madai mashabiki wa Simba walimpiga na chupa mchezaji mwenzao mmoja, Emad El-Nahhas.
KOMBE LA CAF/SHIRIKISHO:
MWAKA 1993ROBO FAINALI:
Simba Vs USM El Harrach (Algeria) 3-0 0-2 3-2
MWAKA 2010:
RAUNDI YA PILI:Aprili 25: Simba Vs Haras El Hodoud 2-1
Mei 8: Haras El Hodood Vs Simba SC 5 – 1
Machi 25, 2012:
RAUNDI YA PILISimba SC 2-0 ES Setif
0 comments:
Post a Comment