Mgosi |
MUSSA Hassan Mgosi, anatarajiwa kuiongoza Daring Club Motema
katika mechi kali ya Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi
ya Tout Puissant Mazembe Aprili 1, mwaka huu.
Hata hivyo, siku hiyo Mussa hatamshuhudia mshambuliaji mwenzake
wa zamani wa Simba SC, Mbwana Ally Samatta ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Lakini Mussa anaweza kupishana pishana uwanjani na kiungo
Mganda, Patrick Ochan ambaye alikuwa naye Simba SC mwaka jana kabla ya wote
kuhamia DRC.
Katika mechi hiyo itakauopigwa kwenye Uwanja wa Stade
Kibassa Maliba, Lubumbashi- Mussa pia anaweza kukutana uwanjani na Mtanzania
mwenzake, Thomas Ulimwengu anayechezea TPM, ingawa bado si mchezaji wa kudumu
kikosi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment