Mussa Mgosi |
Samatta wa nne kutoka kushoto na kikosi cha TP Mazembe |
DC Motema Pembe, klabu inayobebwa na mshambuliaji wa
Kitanzania, Mussa Hassan Mgosi hivi sasa ndio inaongoza Ligi Kuu ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Timu hiyo ya mfungaji bora wa zamani wa Ligi Kuu hadi jana
ilikuwa imekwishacheza mechi tatu, kushinda mbili na sare moja hivyo ina pointi
saba.
Katika mechi ya kwanza, DCMP iliifunga Elima 2-0 ugenini na
mechi ya pili iliifunga Saint-Luc 3-1 kabla ya kutoa sare ya bila kufungana na Makiso
Jumatano.
Wababe hao wa Simba katika Kombe la Shirikisho mwaka jana, kesho
wanashuka tena dimbani kumenyana na Muungano.
Timu nyingine katika Ligi Kuu ya DRC yenye washambuliaji
wawili chipukizi wa Kitanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu na Mbwana Ally
Samatta, Tout Puissant Mazembe inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake sita,
ingawa yenyewe imecheza mechi mbili tu.
Mechi ya kwanza ilishinda 5-0 dhidi ya Tshinkunku na ya pili
1-0 dhidi ya Sanga Balende, wakati leo inamenyana na Molunge.
Machi 22, TP Mazembe itaanza kampeni zake za kuwania taji la
tano la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kumenyana na Power Dynamos ya Zimbabwe
mechi ya kwanza wakicheza ugenini kabla ya kurudiana nyumbani Lubumbashi wiki
mbili baadaye.
0 comments:
Post a Comment