MABAO ya Xavi aliyefunga
kwa mpira wa adhabu na linguine la Lionel Messi yalitosha kuipa Barcelona ushindi
wa 2-0 jana dhidi ya Sevilla na kupunguza idadi ya pointi wanazozidwa na Real
Madrid.
Xavi alipiga bao hilo dakika ya 18 na Mwanasoka Bora wa Dunia,
Messi akafunga bao lake la 31 kwenye La Liga msimu huu baadaye kidogo.
Mabingwa hao watetezi sasa wana pointi 63 kutokana na mechi 27,
wakati Jose Mourinho ameiweka kileleni kwa mbali Real, yenye pointi 70 na leo
inaweza kutudisha pointi 10 za kuizidi Barca iwapo itashinda dhidi ya Malaga Uwanja
wa Bernabeu.
Katika mechi nyingine, Osasuna ilipanda hadi nafasi ya tano
kwa kufikisha pointi 39 baada ya kupata
bao la kusawazisha dakika za lala salama na kufanya sare ya 1-1 na Real
Zaragoza.
Rayo Vallecano ilipanda hadi nafasi ya nane kwa kufikisha
pointi 37 baada ya kuifunga Real Betis 3-0. Zaragoza inabakiwa nafasi ya 20 kwa
pointi zake 19.
0 comments:
Post a Comment