// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MESSI ASEMA MAMBO YOTE SIFA ZIMUENDEE PEP - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MESSI ASEMA MAMBO YOTE SIFA ZIMUENDEE PEP - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 12, 2012

    MESSI ASEMA MAMBO YOTE SIFA ZIMUENDEE PEP

    AKIWA mbioni kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Barcelona,Lionel Messi amesema kwamba mafanikio yake ya siku za karibuni yametokana na kocha Pep Guardiola, ambaye tangu kuwasili kwake Camp Nou yeye amekuwa akipiga sana mabao ikiwemo matano peke yake wiki iliyopita katika mechi moja.
    Baada ya mabao hayo matano Messi katika Ligi ya Mabingwa, amepiga tena mawili Jumatano katika ushindi wa 2-0  dhidi ya Racing Santander na sasa amebakiza mabao matano tu afikie rekodi ya mfungaji bora wa kihistoria wa klabu hiyo, Cesar Rodriguez.
    Cesar ameweka rekodi ya kufunga mabao 235 katika miaka 16 ya kuichezea Barca, lakini Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 24 ana mechi 15 msimu huu za kuvunja rekodi hiyo. Mabingwa hao wa Ulaya na Hispania wanacheza na Sevilla katik La Liga Jumamosi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI ASEMA MAMBO YOTE SIFA ZIMUENDEE PEP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top