// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MESSI APIGA 5 BARCA IKIUA 7, TIMU YA KANIKI YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MESSI APIGA 5 BARCA IKIUA 7, TIMU YA KANIKI YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 08, 2012

    MESSI APIGA 5 BARCA IKIUA 7, TIMU YA KANIKI YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA


    Messi wa pili kutoka kushoto

    MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amezidi kudhihirisha ubora wake katika kizazi cha sasa cha soka, kwa kuwekia rekodi nyingine kwa Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa usiku wa jana, wakati APOEL ilipofanya maajabu makubwa kwa kuitoa Lyon kwa penalti.
    Messi ameibuka mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano katika Ligi ya Mabingwa wakati Barcelona ikiitandika Leverkusen mabao 7-1 kwenye Uwanja wa Camp Noun a kutengeneza ushindi wa jumla mabao 10-2 katika hatua ya 16 bora na kutoa onyo kwa wapinzani wao mbele ya safari.
    “Ni mchezaji bora katika historia ya soka ya dunia na hatujawahi kumuona mwingine kama yeye,” alisema kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas kuhusu Messi.
    Wakati huo huo APOEL, imesonga mbele kimaajabu kweli kweli, ikiitandika Lyon ya Ufaransa mabao 4-3 kwa penalti baada ya ushindi wao wa 1-0 jana kufanya sare ya jumla ya 1-1.
    Kipa wa APOEL iliyow3ahi kumtaka Joseph Kanikio akiwa Simba mwaka 2004, Dionisios Chiotis aliokoa penalti mbili za Lyon na kuiwezesha timu hiyo kung’ara.
    Messi alikuwa hashikiki, alifunga mabao mawili kipindi cha kwanzana matatu kipindi cha pili na kufikisha mabao 49 kwenye mashindano yote— hivyo kuungana na Alfredo di Stefano katika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa kihistoria ya Kombe hilo la Ulaya.
    Akiwa amefikisha mabao 12 msimu huu, mshambuliaji huyo wa Kiargentina amefikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa  Manchester United na Real Madrid, Ruud van Nistelrooy.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI APIGA 5 BARCA IKIUA 7, TIMU YA KANIKI YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top