MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amesimamishwa kwa mara
ya kwanza katika La Liga tangu aanze kuichezea Barcelona, wakati yakie
inatarajiwa kuendelea na kampeni za kuwafukua vinara wa ligi hiyo, Real Madrid kwa
kuwakaribisha vibonde Sporting Gijon Jumamosi.
Mwanasoka huyo bora mara tatu duniani, alilimwa kadi ya tano
ya njano katika mechi dhidi ya Atletico Madrid Jumapili, akiiwezesha Barca kushinda
kwa mbinde 2-1 na atakosa mechi ya kwanza hya ligi msimu huu.
Messi ni kinara wa mabao wa Barca msimu huu, akiwa amefunga
mabao 43 katika mashindano yote – pia aliifungia Argentina mabao matatu peke yake
katika mchezo wa kirafiki Jumatano- lakini wachezaji wenzake watalazimika kupigania
ushindi bila yeye Nou Camp.
Kikosi cha Pep Guardiola hakistahili kupigwa tena ili
kutojiongezea pengo la pointi na Real Madrid, ambao wameshinda mechi zao 19 kati
ya 20 zilizopita.
The Catalans wamefufua matumaini ya kutwaa taji la nne
mfululizo la la Liga, lakini wanazidiwa kwa pointi 10 na wapinzani wao wa jadi,
zikiwa zimesalia mechi 14.
Wanaweza kupunguza pengo hilo na kubaki pointi saba tu, japo
kwa saa 24 kabla ya Real kuivaa Espanyol Jumapili.
Sporting inashika nafasi ya 19 na inahitaji pointi sita ili
kujiweka salama na wametoa sare mechi zao mbili zilizopita tangu wampate kocha
Javier Clemente mwezi uliopita.
Babu huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye alimfundisha Guardiola
katika timu ya taifa ya Hispania, wiki iliyopita aliwakandia Barca akisema
hatarajii kama watatwaa ubingwa.
Real watakuwa wenyeji wa Espanyol wanaoshika nafasi ya nane,
wakati Jose Mourinho atakapokutana na nyodo za mashabiki wa Bernabeu.
Kocha huyo Mreno alipigwa picha London wiki hii na vyombo
vya habari vimeripoti alikuwa ananunua nyumba, ambayo inamanaanisha tetesi za
kurejea kwake nchini humo zinaweza kuwa kweli na anaweza kuitema Real mwishoni
mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment