Walter Mazzari |
KOCHA wa Napoli, Walter Mazzarri atakaa kwenye benchi kesho
kuiongoza klabu yake katika mechi ya marudiano, hatua ya 16 bora Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea, baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya FIFA
kusitisha adhabu yake ya kukosa mechi ya pili, imesema taarifa ya klabu hiyo
leo.
Mazzarri alikosa mechi ya kwanza dhidi ya Chelsea ambayo Napoli
ilishinda 3-1, baada ya Uefa kumfungia mechi mbili kwa kumsukuma mpinzani wake
katika mechi dhidi ya Villarreal.
Kocha huyo maarufu Serie A kwa mkato wake wa nywele, amefanya
kazi kubwa kuirudisha kwenye chati klabu hiyo ya Naples na kesho atakuwa na
mtihani kwenye Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Stamford Bridge ambao akifanikiwa
sambamba na Inter Milan ambao watamenyana na Olympique Marseille ya Ufaransa, ina
maana Italia itaingiza timu tatu Robo Fainali na England watakuwa kapa.
0 comments:
Post a Comment