KAMATI ya Mashindano ya klabu ya Yanga, leo imewapa wachezaji
wa klabu hiyo Sh. Milioni 5 wagawane na kuwaahidi Sh. Milioni 5 nyingine
wakishinda mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzaania Bara unatarajiwa kuwa
mkali na wa kusisimua, kwani Coastal inayofundishwa na wachezaji wawili wa
kimataifa wa zamani nchini, beki Jamhuri Mussa Kihwelo na Juma Ramadhan Mgunda
imepania kushinda kuitibulia Yanga harakati za ubingwa. Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu ameaimbia bongostaz muda
mchache uliopita kwamba morali kuelekea mchezo huo ni kubwa mno na Yanga
wamejipanga sawasawa kuhakikisha wanavuna pointi tatu.Sendeu alisema kwamba Yanga imefanya mazoezi Uwanja wa Kaunda
leo na jana ilifanya Uwanja wa Tiper, Kigamboni wakati juzi ilifanya Uwanja wa
Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.Alipoulizwa sababu za kubadilisha viwanja mara kwa mara,
Sendeu alisema kwamba kocha wao, Mserbia Kostadin Bozidar Papic amekuwa
akilalamikia ubovu katika viwanja vingi wanavyokwenda.Sendeu alisema kwamba Papic anaridhishwa zaidi na Uwanja wa
shule ya sekondari Loyola, Mabibo, Dar es Salaam, ambao kwa sasa umefungwa kwa
ajili ya ukarabati.“Anapapenda pale kwa sababu pia watu hawaangalii mazoezi,
kuna uzio. Kwa hiyo anakuwa huru zaidi na kazi zake,”alisema.Kuhusu hali ya wachezaji, alisema ni Salum Abdul Telela pekee
ambaye hatajumuishwa kwenye mchezo huo kwa sababu amepewa mapumziko baada ya
kupona.“Huo ndio utaratibu wetu kwa sasa, mchezaji akipona anapewa
muda zaidi wa kupumzika awe sawasawa, hata Yae Berko amekaa nje muda mrefu kwa
sababu alipewa na siku za kupumzika,” alisema.Kuhusu wachezaji watakaokwenda Tanga, Sendeu alisema kwamba
hadi sasa hawajaamua lakini watakuwa kati ya 20 na 25.Alisema hiyo inatokana na kwamba, wanasubiri Kikao cha Kamati
ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kinachofanyika
leo, ili waamue.Alisema hiyo inatokana na kwamba kikao hicho kinashikilia
hatima ya wachezaji wao watano, waliositishiwa adhabu na Kamati hiyo iliyo
chini ya Mwenyekiti Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Alfred
Tibaigana baada ya kufungiwa awali na kamati ya Ligi Kuu, hivyo kama
watarejeshwa ‘rumande’ ina maana hawatakwenda Tanga.Kamati ya Tibaigana iliwaachia huru wachezji watano wa Yanga
waliokuwa wamefungiwa kwa vipindi tofauti na Kamati ya Ligi ya TFF, baada ya kuridhika
na utetezi wa klabu hiyo juu ya adhabu hizo.Akitangaza kusitisha adhabu hiyo, Tibaigana alisema kwa
mujibu wa taratibu za TFF, Kamati ya Ligi haina mamlaka ya kumfungia mchezaji yeyote
wala kutoa adhabu, isipokuwa Kamati ya Nidhamu.Kamati ya Ligi iliyokutana Machi 12, mwaka huu chini ya Mwenyekiti
wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ iliwafungia wachezaji hao wa Yanga kwa tuhuma za
utovu wa nidhamu walioufanya kwenye mechi ya Azam FC, Machi 10, mwaka huu,
Uwanja wa Taifa.Mabeki Stefano Mwasika aliyempiga ngumi refa Israel Nkongo alifungiwa
mwaka mmoja na faini ya Sh Milioni 1, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alifungiwa mechi
sita na faini ya Sh. 500,000, viungo Nurdin Bakari alifungiwa mechi tatu na
faini Sh. 500,000 sawa na Omega Seme na mshambuliaji Jerry Tegete.Akiizungumzia mechi na Coastal Union, Sendeu alisema morali
ni kubwa na wanaamini wanakwenda kuchukua pointi tatu huko.Alisema timu itaondoka mapema kesho na tayari mjini Tanga
wamekwishaandaliwa mazingira ya sehemu salama ya kufikia, kufanya mazoezi na
hata kula, ili kuhepa fitina za Wagosi ambao wamepania kweli kuiadhiri Yanga, kulipa
kisasi cha 5-1 walizofungwa katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Samuel Eto’o eyes CAF Exco seat
-
Cameroonian Football Football (FECAFOOT) president Samuel Eto’o is keen to
become a member of the Confederation of African Football (CAF)’s executive
com...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment