// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MASHUJAA WAPYA KUTAMBULISHWA NYUMBANI LOUNGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MASHUJAA WAPYA KUTAMBULISHWA NYUMBANI LOUNGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 06, 2012

    MASHUJAA WAPYA KUTAMBULISHWA NYUMBANI LOUNGE


    Chaz Baba, nyota wa bendi ya Mashujaa

    ONYESHO maalum la utambulisho wa wasanii wapya waliojiunga na bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Band, mnenguaji Lilian Tungaraza ‘Internet’ na mpapasa Kinanda Ally Akida linatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
    Internet aliyekuwa akifanya kazi katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Akida aliyerkuwa mwanamuziki wa kujitegemea walijunga na MAshujaa wiki iliyopita baada ya kusaini mktaba wa miaka miwili.
    Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Mashujaa Musica Maxi Luhanga alisema mandalizi ya onyesho hilo yamekamilika hivyo amaewaomba mashabiki wa muziki wa dansi kujitokeza kwa wingiu.
    Alisema mbali na bendi ya Mashujaa , onyesho hilo pia litapambwa na Machozi Band inayomilikiwa na Mwanadada Lady Jay Dee ambapo kutakuwa na mambo mazuri ya kuvutia.
    “Si onyesho la kukosa kwa mpenda muziki wa dansi kwani pamoja na utambulisho wa wasanii wetu wapya, bendi hizi zinatarajiwa kukonga kwa nyimbo zake kadhaa sambamba na shoo ya nguvu toka katika sdafu zao za unenguaji,”Alisema Luhanga.
    Naye Lilian akizungumzia hatua ya kuhamia kwake Mashujaa alisema kilichompeleka huko ni maslahi mazuri mazuri anayolipwa kwa kazi yake sambamba na fedha ya kujikimu kwa masuala mbalimbali ikiwemo matibabu, usafiri na nyumba.
    Alisema pamoja na hilo amekwenda huko kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi katika harakati zake hizo za kusaka maisha kupitia muziki huku akiwaahidi mambo makubwa mashabiki wa bendi hiyo na muziki wa dansi kwa ujumla.
    Internet amekuwa msanii wa pili kunyakuliwa na Mashujaa Musica hivi karibuni toka Twanga Pepeta ambayo mapema mwaka huu ilimchukua mwimbaji Charles Gabriel ‘Charlz Baba’ kwa lengo la kuimarisha kundi lao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA WAPYA KUTAMBULISHWA NYUMBANI LOUNGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top