Bakitelli kulia na Mancini kushoto |
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema katika vita
kali ya ubingwa wa Ligi Kuu England, hamuamini Mario Balotelli.
Kocha huyo Mtaliano, ambaye mfungaji wake bora Sergio Aguero ameumia
mguu wiki hii, anakabiliwa na tatizo la washambuliaji kwani Edin Dzeko ndiye
pekee aliyefunga mabao mawili katika mechi 17 zilizopita na Carlos Tevez ndio
kwanza anarejea taratibu katika kiwango chake baada ya miezi mitatu ya kuwa likizo
ya kujitakia kwao Argentina.
Na mzigo huo unamuangukia Balotelli, pamoja na hayo Mancini hana
uhakika kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anaweza kuaminiwa katika
patashika ngumu ya mbio za ubingwa.
"Simuamini Mario, lakini yupo hivi. Sifikiri kama yeyote
anaweza kumuamini Mario," aliwaambia waandishi wa Habari. "Anaweza
kufunga mabao mawili kwa urahisi kesho au katika mchezo mwingine na Arsenal. Lakini
hatuwezi kumuamini."
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 hana shaka na uwezo wa
mchezaji huyo wa zamani wa Inter, lakini swali ni juu ya kiwango mchake katika
mechi za karibuni tangu amtoe nje kipindi cha pili mchezo katika wa City na
Chelsea.
"Ni mchezaji babu kubwa, anaweza kufanya kitu chochote
mchezoni. Anaweza kufunga mabao matatu, lakini pia anaweza kupewa kadi nyekundu.
"Ni kazi yake, anatakiwa kufanya kazi, anatakiwa
kupumzika, lakini ni mdogo. Ninatumaini anaweza kufunga mabao matano au sita
muhimu katika mechi nane zilizobaki.
"Nilistaajabishwa na kiwango chake katika mechi na Chelsea,
lakini si dhidi ya Stoke," alisema.
Wawili hao walipigwa picha pamoja mapema wiki hii wakibishana,
lakini mchezaji huyo wa zamani wa Sampdoria alipuuza madai hayo.
alisema: “Nilizungumza naye kwenye mazoezi kwa sababu
nilikuwa namfafanulia kitu fulani uwanjani, ni hivyo tu.”
Lakini kulikuwa kuna matatizo zaidi kwa Mancini wiki hii, wakati
Balotelli aliporejea Milan katika siku zake mbili za mapumziko.
Nyota huyo mzaliwa wa Sicily, alivamia Mkutano na Waandishi
wa Habari wa kumtambulisha kocha mpya wa Inter kumsalimia kocha huyo Andrea
Stramaccioni, ambaye amechukua nafasi ya Claudio Ranieri na kusabab isha usumbufu.
Pamoja na hayo, Mancini anatumainin kwamba mchezaji huyo
mwenye thamani ya pauni milioni 20 anaweza kutumia muda wake mwingi kukua taratibu.
"Siwezi kumchukua na kumfungia nyumbani kwake kwa siku
mbili! Dhahiri wakati utafika atakapokuwa anaelewa nini anatakiwa kufanya
anapopewa mapumziko ya siku mbili.
"Natumaini anakua, kwa sababu anatakiwa kujirekebisha."
0 comments:
Post a Comment