Rooney aliye katika kiwango cha juu, ataibeba united leo? |
AKIWA hana majeruhi kikosini, Sir Alex Ferguson hana
wasiwasi na leo anatarajiwa kushusha mziki mzito katika mechi na Fulham, ingawa
Paul Scholes anaweza kupumzishwa katika mechi dhidi ya wapinzani wao hao wenye
rekodi nzuri ya asili Uwanja wa Old Trafford.
Fulham imethibitisha mapema wiki hii wachezaji pekee
wanaoweza kukosa safari ya Old Trafford wanaweza kuwa Orlando Sa, Zdenek
Grygera na Steve Sidwell. Katika wiki za karibuni wamekuwa wakicheza mfumo wa kushambulia zaidi, huku Dembele akiingia ndani na Pavel Pogrebnyak na Andrew Johnson wanasimama mbele wote.
Lakini leo dhidi ya mabingwa watetezi Uwanja wa Old Trafford, wanatarajiwa kujaza watu katika nafasi ya kiungo akina Danny Murphy na Mahamadou Diarra, na Dembele katika eneo la ushambuliaji.
JE WAJUA?
•Bao la mwisho Fulham kufunga katika Uwanja wa Old Trafford lilikuwa
mwaka 2006, tena Rio Ferdinand akijifunga.
•Manchester United imefunga
penalti tisa msimu huu, ambazo ni nyingi katika Ligi Kuu.
•Wayne Rooney amefunga
mabao 16 katika mechi zake 16 zilizopita United kwenye michuano yote.
•Rooney pia amefunga
mabao matano katika mechi nne zilizopita dhidi ya Fulham Uwanja wa Old
Trafford.
•Martin Jol hajawahi
kuifunga Manchester United katika Ligi Kuu akiwa kocha. Baada ya kutoa sare
katika mechi zake mbili za mwanzo dhidi yao, alifungwa nyingine saba.
•Pavel Pogrebnyak ameifunga
matano Fulham katika mashuti matano yaliyokwenda sawa.
• David Silva pekee
ametoa pasi nyingi za mabao zaidi ya Antonio Valencia msimu huu, akitengeneza 12
dhidi ya 11 za winga huyo wa United.
•Timu zote zipo
kwenye kundi la timu nne zilizofunga mabao zaidi ya matano kwenye mechi moja
msimu huu - United ikizifunga Arsenal 8-2 na Fulham ikiichapa QPR 6-0. Timu
nyingine kwenye kundi hilo ni Arsenal na Manchester City.
•Tangu United itoe
sare ya 3-3 na Chelsea, wameshinda mechi tano mfululizo za ligi. Pamoja na
hayo, katika kipindi hicho wamepoteza mechi tatu katika mashindano yote, zikiwemo
mbili za Europa League.
VIKOSI VYA LEO:
MANCHESTER UNITED:
De Gea, Rafael, Evans, Ferdinand, Evra, Valencia, Carrick, Giggs, Young, Welbeck
na Rooney.
FULHAM: Schwarzer,
Kelly, Senderos, Hangeland, Riise, Murphy, Diarra, Duff, Dempsey, Dembele na Pogrebnyak.
0 comments:
Post a Comment