MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City ya England imetolewa katika Europa
League kwa hasara ya mabao ya ugenini licha ya ushindi wake wa jana usiku wa
mabao 3-2 dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno.
Matias Fernandez alifunga dakika ya 33 kwa mpira wa adhabu na
Ricky van Wolfswinkel akafunga tena
dakika ya 40 kuunenepesha ushindi wa Wareno wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza.
Ikihitaji mabao manne ili kusonga mbele, City ilionekana kama
kuzinduka kwa mabao ya Sergio Aguero dakika ya 60 na 82, yaliyofuatiwa na bao
la Mario Balotelli dakika ya 75 na kufanya sare ya jumla ya mabao 3-3.
Lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa uwezo wao kwenye Uwanja wa
Eithad na mwanzo wa safari ya kuiaga michuano ya Ulaya mwaka huu.
“Ninajivunia kiwango, (lakini) nimestaajabishwa na mechi hizi
mbili, kwa sababu nafikiri kwa mechi zote mbili, hatustahili kusonga mbele,” alisema
kocha wa City, Roberto Mancini.
Matokeo hayo yanamaanisha England hawatakuwa na timu hata
moja kwenye Robo Fainali ya michuano hiyo, kufuatia Manchester United kutolewa
na Athletic Bilbao mapema jana.
0 comments:
Post a Comment