// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN CITY, MAN UNITED ZINA MZIGO MZITO ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN CITY, MAN UNITED ZINA MZIGO MZITO ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    MAN CITY, MAN UNITED ZINA MZIGO MZITO ULAYA


    Wayne Rooney ataibeba United leo?
    WAPINZANI wa jiji la Manchester, United na City wako kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini wako mguu nje, mgjuu ndani kwenye Europa League.
    United itakuwa ugenini ikijaribu kulipa kisasi cha 3-2 mbele ya Athletic Bilbao kesho.
    Hofu ni kwamba wachezaji makinda wa Bilbao waliifunika ile mbaya United kwenye mchezo wa kwanza na wengi wanaamini ndoto za Mashetani hao Wekundu kubeba taji lolote la Uaya zitazimwa kesho.
    Angalau City watakuwa kwenye ardhi ya nyumbani ambako haijafungwa kwenye michuano ya Ulaya kwa miaka minne, lakini watatakiwa kulipa kisasi cha 1-0 kutoka kwa Sporting Lisbon wiki iliyopita.
    Bilbao inawania kuwa moja ya timu tatu za Hispania zilizotinga Robo Fainali, nyingine zikiwa ni Atletico Madrid na Valencia zote zina faida ya mabao mawili kutoka mechi za kwanza.
    Olympiakos, Twente na AZ Alkmaar zote zina nafasi ya kusonga mbele zikiingia kwenye mechi za marudiano.
    Hii ni mara kwanza kwa Manchester United kupoteza mechi mfululizo katika michuano ya Ulaya ndani ya miaka 16, kufuatia kutolewa Ligi ya Mabingwa.
    “Tumekuwa tuna mwaka mbaya Ulaya,” alisema kocha wa United, Alex Ferguson said.
    Wachezaji wa United, Nani, Anderson anayesumbuliwa na nyama za paja kama Antonio Valencia na Tom Cleverley anayeumwa kifundo cha mguu wote wako shakani kucheza mechi hiyo ya Europa League, wakati Wayne Rooney anatarajiwa kupiga kazi, ingawa mwishoni mwa wiki wanakabiliwa na mchezo wa ligi dhidi ya Wolves.
    Mshambuliaji wa Bilbao, Fernando Llorente na kiungo mchezeshaji Oscar de Marcos wote walikosa mazoezi mapema wiki hii kuelekea kwenye mechi hii itakayopigwa Uwanja wa San Mames, wenye uwezo wa kumeza mashabiki 40,000.
    Bilbao inawania kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1976-77.
    Manchester City watakaoshuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kwenye Ligi Kuu Jumapili, kuna tetesi kwamba watamchezesha Carlos Tevez.
    Lakini safu ya ulinzi ya City itaendelea kuwakosa majeruhi Vincent Kompany (calf) na Joleon Lescott (nyonga) na beki wa kulia, Pablo Zabaleta (nyama za paja).
    Aidha, Phillip Cocu ataanza rasmi kazi yake ya ukocha PSV akiiongoza timu hiyo ya Uholanzi kujaribu kulipa kisasi cha 4-2 kutoka kwa Valencia na kufuta gundu la kufungwa mechi tatu mfululizo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY, MAN UNITED ZINA MZIGO MZITO ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top