Torres |
Theo |
Mwokozi wa Manchester City, Aleksandar Kolarov |
KLABU ya Manchester City leo imepata mabao mawili ndani ya
dakika sita za mwisho na kubahatisha sare ya 3-3 na Sunderland na kutunza
rekodi yao ya kutofungwa nyumbani katika miezi 15 kwenye Ligi Kuu ya England.
City ilitaka kuwatia presha vinara wa ligi hiyo, Manchester
United lakini Sebastian Larsson akawafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 31.
Mario Balotelli alisawazisha kwa penalti dakika ya 43, lakini
Nicklas Bendtner akaifungia la pili Sunderland dakika mbili baadaye na Larsson
akafanya 3-1 dakika ya 55.
Balotelli akafunga tena dakika ya 85 na Aleksandar Kolarov akasawazisha
dakika moja baadaye.
City haijafungwa kwenye Uwanja wa Etihad tangu Desemba 2010 ilipopigwa 2-1 na Everton, lakini.
Katika mchezo mwingine, rekodi ya Arsenal kushinda mechi saba
mfululizo katika Ligi Kuu imevunjwa leo na QPR kwa kichapo cha 2-1 Uwanja wa
Loftus Road.
Rangers iliyokuwa imeshinda mechi mbili tu katika mechi 18, mabao
yake leo yalifungwa na Adel Taarabt na Samba Diakite, wakati la Arsenal lilifungwa
na Theo Walcott.
Chelsea nayo imeshinda 4-2 dhidi ya Aston Villa.
Villa ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2
zikiwa zimebaki dakika 10, lakini Branislav Ivanovic akafunga bao lake la pili
kwenye mchezo huo na Fernando Torres akafunga lingine dakika za lala salama kuipa
matumaini Chelsea inayoshika nafasi ya tano ya kumaliza ligi ndani ya Top Four.
Daniel Sturridge aliifungia Chelsea bao la kuongoza na Ivanovic akapiga la pili dakika ya 51 kabla
ya James Collins na Eric Lichaj kuifungia Villa.
Nahodha wa Villa, Stiliyan Petrov aliushuhudia mchezo huo
akiwa jukwaani siku moja baada ya kutangazwa anaumwa acute leukemia.
0 comments:
Post a Comment