MAFISANGO ASIMAMISHWA MUDA USIOJULIKANA , KABURU AMWAGA FEDHA KAMBINI SIMBA
Mafisango aliyebebwa juu na wachezaji wenzake baada ya kufungta bao, je kukosekana kwake hakutaiathiri timu?
UONGOZI wa Simba umemsimamisha kwa muda usiojulikana kiungo
wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango kwa utovu wa nidhamu,
imeelezwa.Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba,
Mafisango amechukuliwa hatua hiyo kwa utovu wa nidhamu, ambao umekuwa
ukijirudia mara kwa mara.Wakati huo huo, mgomo wa wachezaji wa Simba kuhusu mgawo wao
baada ya mechi dhidi ya ES Setif ya Algeria umeisha baada ya Makamu Mwenyekiti
wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kwenda kuwaongezea fedha wachezaji wa
timu hiyo.Simba ipo kambini Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam ikijiandaa
na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya African Lyon Jumamosi mjini Dar es Salaam.Baada ya mechi hiyo, Simba itaelekea Algeria kwa ajili ya
mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Se Setif, wakipitia Misri.
Samuel Eto’o eyes CAF Exco seat
-
Cameroonian Football Football (FECAFOOT) president Samuel Eto’o is keen to
become a member of the Confederation of African Football (CAF)’s executive
com...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment