KLABU ya Liverpool inaweza kufurahi vikombe kadhaa, lakini
safari yao kuelekea QPR imebeba mustakabali wao katika Ligi Kuu ya England kama
wanaweza kurejea kwenye chati.
Wekundu hao, tayari wametinga Nusu Fainali ya Kombe la FA, ambako
watakutana na ama Everton au Sunderland, baada ya kuifunga 2-1 Stoke Jumapili.
Timu ya Kenny Dalglish tayari imetwaa taji lake la kwanza ndani ya miaka sita, kwa kuifunga Cardiff ya Daraja la Kwanza kwa penalti kwen ye fainali ya Kombe la Ligi.
Matokeo hayo mazuri ni tofauti kabisa kwenye Ligi Kuu, ambako wanashika nafasi ya saba, wakizidiwa pointi 10 na Arsenal inayoshika nafasi ya nne na wanaizidi pointi tatu tu Swansea iliyopanda msimu huu.
Klabu hiyo ya Anfield, tayari imemaliza misimu miwili ikiwa nje ya Ligi ya Mabingwa na iko hatarini na kumaliza nje ya Nne Bora kwa mwaka wa tatu mfululizo.

0 comments:
Post a Comment