// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOCHA WA 15 ATIMULIWA NDANI YA MSIMU MMOJA SERIE A - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOCHA WA 15 ATIMULIWA NDANI YA MSIMU MMOJA SERIE A - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    KOCHA WA 15 ATIMULIWA NDANI YA MSIMU MMOJA SERIE A


    Davide Ballardini 
    KUFUKUZWA kwa Davide Ballardini Cagliari Jumapili kunamfanya awe kocha wa 15 katika ligi inayoshirikisha timu 20, Serie A kufukuzwa msimu huu.
    Italia kwa haraka inageuka kuwa tanuri la makocha kwa marais wa klabu kuwatupia virago mara moja, wanapoona timu zao haziendi vizuri.
    Rais wa Cagliari, Massimo Cellino amefukuza kocha wa tatu katika kipindi kisichozidi miezi saba.
    Agosti katika kujiandaa na msimu mpya, Sardinians walikuwa wanafundishwa na kocha wa zamani wa Italia, Roberto Donadoni alifukuzwa baada ya mechi ya kirafiki ambayo Cagliari pamoja na kushinda, lakini akaondolewa na Massimo Ficcadenti akachukua nafasi.
    Alidumu kwa miezi isiyozidi mitatu kabla ya Ballardini kuchukua nafasi, ambaye anafukuzwa ndani ya miezi mine na Ficcadenti akipewa nafasi kubwa ya kurudishwa kazini.
    Miaka michache iliyopita, kocha wa sasa wa Udinese, Francesco Guidolin alidumu kwa miaka minne Palermo kati ya 2004 na 2007.
    Kufukuzwa kwa Ballardini kunamaanisha Ligi Kuu ya Italia ndio inaongoza kubadilisha makocha zaidi ya England iliyobadili wanne hadi sasa, Ujerumani (sita) na Ufaransa (wanne).
    La Liga nayo inatisha kwa kufukuza makocha, ikiwa imefukuza makocha tisa hadi sasa.
    Chini ya Cagliari, ambayo inasaka kocha wan ne msimu huu, kuna Palermo, Cesena na Novara ambao wako tayari kwa mechi ya tatu wakati klabu nyingine sita zimefukuza makocha iliyoanza nao msimu huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA WA 15 ATIMULIWA NDANI YA MSIMU MMOJA SERIE A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top