MUSTAKABALI wa Michael Essien katika klabu ya Chelsea
hautaamuliwa hadi klabu hiyo imtaje kocha wake mpya, hiyo ni kwa mujibu wa
wakala wa mchezaji huyo.
Kwa sasa Roberto Di Matteo ni kocha wa muda hadi mwsihoni
mwa msimu, wakati kocha mpya atatajwa kwa ajili ya kuanza kazi msimu ujao.
Wakati mustakabali wake ukiwa haueleweki, tayari tetesi
zimeanza kuzagaa kwamba kiungo huyo atatimkia Italy kwa vigogo wa Serie A,
Juventus.
Mghana huyo mwenyr umri wa miaka 29 amekuwa akiandamwa na
majeruhi msimu huu Stamford Bridge, jambo ambalo mwishowe limeshusha kiwango
chake.
Pamoja na hayo, wakala wa mchezaji huyo aliyenmkana baba
yake mwaka jana, Fabien Piveteau amesema hakuna kitakachoamuliwa juu ya
mustakabali wa mteja wake hadi kocha mpya ateuliwe.
“Hadi sasa hakuna kituna sijasikia chochote kutoka klabu ya
Italia.
"Ana furaha Chelsea? Amepitia wakati mgumu, lakini tu
kwa sababu ametoka kwenye maumivu makali.
"Nimezungumza na Chelsea na wamesema wana furaha, lakini
kwenye soka huwezi kujihakikishia nini kitatokea baadaye.
“Bado ana miaka mitatu katika mkatabva wake, lakini itategemea
na nani atakuwa kocha Chelsea mwishoni mwa msimu."alisema.
0 comments:
Post a Comment