// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KLABU ULAYA ZAGOMBEA JEMBE LA PARAGUAY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KLABU ULAYA ZAGOMBEA JEMBE LA PARAGUAY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    KLABU ULAYA ZAGOMBEA JEMBE LA PARAGUAY


    Caceres kushoto akimdhibiti Neymar
    KIUNGO mkabaji chaguo la kwanza la Paraguay, Victor Caceres anawaniwa na klabu kubwa za Ulaya asajiliwe msimu ujao, kwa mujbiu wa mwakilishi wake.
    Baada ya kucheza soka ya nguvu kwenye Kombe la Dunia 2010 na michuano ya Copa America mwaka jana, Caceres amejipatia umaarufu mkubwa kama miongoni mwa viungo bora wa ulinzi.
    ETSM, kampuni ya uwakala wa michezo yenye maskani yake London, ambayo ina mkataba na Caceres, imethibitisha kwamba vigogo wa Ulaya wameonyesha nia kwa mteja wao, zikiwemo klabu za England ambazo hakuzitaja jina.
    “Wote tunafahamu kwamba Victor Caceres ni mchezaji wa kiwango cha dunia, muhimu zaidi, tunahitaji kufanya uamuzi ambao utakuwa na manufaa kwa manufaa yake binafsi na maendeleo yake," alisema Msemaji wa ETSM.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia anaweza kucheza kama beki wa kati, amekuwa na mafanikio, akitwaa  ubingwa wa Paraguay mara tatu na kucheza mechi zaidi ya 160 katika klabu ya nchini mwake, Libertad.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KLABU ULAYA ZAGOMBEA JEMBE LA PARAGUAY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top