// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIVUMBKI LIGI KUU LA UGANDA CHAANZA TENA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIVUMBKI LIGI KUU LA UGANDA CHAANZA TENA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 09, 2012

    KIVUMBKI LIGI KUU LA UGANDA CHAANZA TENA LEO

    LIGI Kuu ya Uganda, Bell Super League inarejea leo baada ya mapumziko mafupi ya kupisha mechi za kimataifa.
    URA, vinara wa ligi hiyo kwa pointi zao 34, watakutana na Bidco inayoshika nafasi ya 11 kwenye Uwanja wa Lugazi kujaribu kusaka pointi za kuwakimbia Bunnamwaya, wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi zao 33, na Express wenye pointi 32 wanaoshika nafasi ya tatu.
    Bunnamwaya itasafiri hadi Wankulukuku kuwafuata Utoda wanaoshika mkia wakati Express watakwedna Bombo kumenyana na timu ya jeshi, Simba, ambayo inashika nafasi ya 13 kwa pointi zake 16.
    Mechi ya kwanza kati ya Express na Simba iliisha kwa 3-0 timu ya jeshi ikiadhibiwa Uwanja wa Wankulukuku.
    Mechi nyingine mbili leo, mabingwa wa kihistoria Uganda,  SC Villa wenye mataji 16 wataikaribisha George Nsimbe.
    Villa inayonolewa Mike Mutebi ina pointi 22, itakuwa ikipigania ushindi baada ya kuwa imeshinda mechi moja tu katika mechi tatu zilizopita ya mwisho wakitoka sare ya bila kufungana na wapinzani wa jadi, Express.

    LEO IJUMAA MACHI 9, SAA 10.30 JIONI:
    Victors vs Masaka, Kakindu
    URA vs Bidco, Lugazi
    Utoda vs Bunnamwaya, Wankulukuku
    Simba vs Express, Bombo
    SC Villa vs Fire Masters, Nakivubo

    KESHO J’MOSI MACHI 10, 2012 SAA 9:00 ALASIRI:
    Maroons vs Police, Luzira
    Proline vs Water, Nakivubo
    KCC vs Hoima–Busia, Namboole
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIVUMBKI LIGI KUU LA UGANDA CHAANZA TENA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top