Polisi wakimdhibiti shabiki aliyepinda |
ASKARI wa Jeshi na Polisi nchini Misri kwa pamoja
wamepambana na maelfu ya mashabiki wenye hasira huko Suez Canal baada ya
kusimamishwa kwa klabu yao kufuatia tukio la vifo vya mashabiki mwezi uliopita,
mashahiri wamesema leo. Taarifa za kitabibu zimesema kijana mmojua aliuliwa.
Kasheshe la Februari 1 katika mji wa Port Said lililosababisha
vifo vya watu wapatao 73, lilikuwa ni janga kubwa zaidi kwenye soka duniani
ndani ya miaka 15. Viongozi wamefunguliwa mashitaka kuwa kuwashawishi mashabiki wa Port Said kuwashambulia mashabiki wa klabu ya Cairo, ambayo I na historia ndefu ya uadui na Polisi.
Vurugu mpya, askari wa Misri waliwapiga kwa mabomu ya machozi na gesi mashabiki wa Al Masry ya Port Said, ambao walikuwa wanafanya fujo wakida klabu yao na mji haukutendewa haki kw aklabu yao kufungiwa. Vurugu zilianza jioni ya Ijumaa na kuendelea hadi leo.
0 comments:
Post a Comment