// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIMENUKA TENA, KLABU LIGI KUU ZAKUTANA KESHO KUICHENJIA TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIMENUKA TENA, KLABU LIGI KUU ZAKUTANA KESHO KUICHENJIA TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 08, 2012

    KIMENUKA TENA, KLABU LIGI KUU ZAKUTANA KESHO KUICHENJIA TFF


    VIONGOZI wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kesho watakuwa na kikao kizito mjini Dar es Salaam, kujadili ‘changa la macho’ walilopigwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Habari za ndani ambazo bongostaz imezipata kutoka kwa umoja wa klabu za VPL, zimesema kwamba kikao hicho kinafuatia TFF kuwahadaa kuhusu suala la kampuni ya Ligi Kuu.
    Kiongozi mmoja wa klabu, ameiambia bongostaz leo kwamba Kamati ya Ligi Kuu iliyoundwa na TFF haikuwasilisha hoja ya Kampuni katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Februari 12, mwaka huu.
    Kiongozi huyo, alisema mtu ambaye anaingia kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF kutoka kwenye Kamati yao ni Mwenyekiti wao pekee, Wallace Karia.
    “Karia pekee ndiye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye kutoka kwenye Kamati ya Ligi Kuu iliyoundwa na TFF anaingia kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji.
    Lakini ajabu, habari ambazo tumezipata ni kwamba hajawasilisha hoja hiyo na hakuna mtu aliyeinuka kuhoji kuhusu suala la kampuni,” alisema kiongozi huyo.
    Kiongozi huyo, alimlalamikia rais wa TFF pia, Leodegar Chillah Tenga kwamba aliziahidi klabu yeye mwenyewe atasimamia hadi kuhakikisha suala la kampuni linaingia kwenye Kamati ya Utendaji, lakini ajabu ameendesha kikao cha Kamati ya Utendaji bila kujadili kampuni.
    “Mbaya zaidi ni kwamba, sasa wanakwenda kwenye Mkutano Mkuu (utakaohusisha uchaguzi Mkuu pia) bila ajenda ya kampuni,” alilalamika kiongozi huyo.    
    Akiizungumzia Kamati ya Ligi Kuu, kiongozi huyo alisema kwamba ipo kama kivuli na haihusiki na uendeshaji wa Ligi Kuu
    “Karia anaishi nje ya Dar es Salaam, Ofisa waliyesema ataajiriwa, hadi leo hajaajiriwa. Kazi zote zinafanywa na ofisi ya Sadi Kawemba kama zamani,”alisema. 
    Kamati ya Ligi Kuu inaundwa na Wallace Karia (Mwenyekiti), Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti), Damas Ndumbaro, Yahya Ahmed, Meja Charles Mbuge, Steven Mguto, Geoffrey ‘Kaburu’ Nyange, Seif Ahmed, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hemedi Msangi na Henry Kabera (Wajumbe).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIMENUKA TENA, KLABU LIGI KUU ZAKUTANA KESHO KUICHENJIA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top