WACHEZAJI wa klabu ya soka ya Simba
wamegoma kuingia kambini wakishinikiza kulipwa sehemu ya posho zao baada ya
mechi ya kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria jumapili
iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mamapipiro.blogspot.com, jana kikosi cha Simba kilitakiwa
kuingia kambini Bamba Beach kwa ajilio ya kujiandaa na mechi yake ya ligi kuu
bara dhidi ya African Lyon mwishoni mwa wiki lakini baadhi ya wachezaji waligoma
kwenda kambini wakishinikizwa walipwe kwanza posho zao.
Habari zilizopatikana toka ndani ya
klabu hiyo zinaeleza kwamba awali uongozi uliahidi kuwapa shilingi mil.30 lakini
walishangazwa na kupatiwa shilingi mil.15 tena ambazo zilitolewa na mmoja ya
wadau wa klabu hiyo Azim Dewji kama zawadi ya timu hiyo kuwafunga Es Setif mabao
2-0.
Fuatilia mamapipiro.blogspot.com kwa taarifa zaidi
kuhusu sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment