// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIBERA ACHA CHUKI YA KASONGO MPINDA NA MK GROUP - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIBERA ACHA CHUKI YA KASONGO MPINDA NA MK GROUP - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Thursday, March 29, 2012

        KIBERA ACHA CHUKI YA KASONGO MPINDA NA MK GROUP


        Kasongo Mpinda

        WIMBO:-KIBERA ACHA CHUKI
        MTUNZI:-KASONGO MPINDA.”CRYTON”
        WAIMBAJI:-KASONGO MPINDA.
        BENDI:-MK GROUP.”NGULUPA TUPATUPA DANCE”
        KATIKA wimbo huu mbali na ujumbe unaotuasa jamii kuondokana na roha za fihi na chuki huku ukituelekeza kuondokana na ubinafsi bali maisha yetu yanastahili kutawaliwa na upendo; utamkubali mwana mama;Asia Daruweshi kwa jinsi alivyomudu kucheza na kinanda kwa umahili mkubwa.
        Ama utaridhika na sauti yenye msisitizo katika ghani ya mtunzi wa kibao hiki; Nguli Kasongo Mpinda”Cryton”kwa jinsi alivyoichezea kwa kupanda na kushuka huku akiwasilisha Ujumbe endelevu tofauti na vibao vya watunzi wa leo hii hususani wa kizazi kipya ambapo nyimbo zao nyingi hazina maudhui, na pindi upatikanapo basi huwa hasi.
        Mtunzi na Mwimbaji anamkanya muhusika kuondokana na tabia aliyonayo ambayo haina maslahi hapa duniani. Kwani yastahili UCHEKE NA WATU UPATE VIATU. Kinyume na hapo, tabia aliyonayo ya ubinafsi,chuki na roho mbaya atendayo itamletea madhara hapa duniani naaam PELE NDILO LIWALO DONDA!
        Tunakumbushwa kwamba sisi sote ni bin Adamu,yatupasa tupendane asilani tusiwekeane kinyongo.yastahili tusaidizane kwa kila jambo,pindi unapomuona mwenzio yumo kwenye kisima kirefu mpe mkono umvute na si kumnyanyapaa kwa ugumu wa maisha yanayomkabili.
        Tungo hii iliyorekodiwa mnamo mwaka 1986,imefanyiwa kazi inavyostahili na kuleta mvuto kwa msikilizaji,mbali na mtunzi pamoja na “Super Mama;”Asia Daruweshi ni Andy Swebe aliyeungurumisha gitaa zito, Mafumu Bilali “Super Sax”ama Bombenga aliyepuliza Saxaphone, Joseph Mulenga “King Spoiler” aliyepiga gitaa linaloongoza na Monga Stanley”Monga Stan”aliyecheza na gitaa la kati “Rythym;
        Trampet zilipulizwa na Abdallha Tuba na Kayembe Ndalambo,huku Abdallha Rock akikaanga chipsi”Drums”na Tumba  zikiwa katika  himaya za Sidy Moris”Super Conga”

        SASA IMBA:-
        Mpende mwenzioo
        Kama unavyojipenda wewee eeeh!
        Mwenye upendoo
        Hana Hasiraa
        Mwenye upendoo ni mtulivuu
        Mwenye upendoo huwatumikia wenzakee
        Upendo ni utumishi
        Utumishi ni upendo
        Upendo ni uhai
        Chuki ni mauti
        Upendo wa kwelii
        Sio wa maneno matupu maamaaaa
        Mbali na matendo maamaaaa
        Mbali na matendooooo oooh!
        {Wee Kiberaa Acha chuki wee..utaleta ugomvi eee}
        Mpende mwenzioo
        Kama unavyojipenda wewee eeeh!
        Mwenye upendoo
        Hana Hasiraa
        Mwenye upendoo ni mtulivuu
        Mwenye upendoo huwatumikia wenzakee
        Upendo ni utumishi
        Utumishi ni upendo
        Upendo ni uhai
        Chuki ni mauti
        Upendo wa kwelii
        Sio wa maneno matupu maamaaaa
        Mbali na matendo maamaaaa
        Mbali na matendooooo oooh!

        CHORUS:-
        Kibera acha chuki eee
        Chuki yaleta uchawii yeeh..
        Kibera acha chuki eee
        Chuki yaleta migonganoo oooh..
        Kibera acha chuki eeeeh…
        Chuki yavunja umoja yeeeh..yooo…Kiberaaa!
        Kibera weee bwana Kiberaaa
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Kibera acha chuki eee
        Chuki yaleta ugomvii yeeh..
        Kibera acha chuki eee
        Chuki yaleta migonganoo oooh..
        Kibera acha chuki eeeeh…
        Chuki yavunja umoja yeeeh..yooo…Kiberaaa!
        Kibera weee bwana Kiberaaa
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Oooo…yooo Kiberaaaa
        Kibera wee bwana Kiberaa…
        Oooo…yeeeh Kiberaa
        Kibera wacha wee Kiberaaaah!

        Kibera acha chuki eee
        Chuki yaleta uchawii yeeh..
        Kibera acha chuki eee
        Chuki yaleta migonganoo oooh..
        Kibera acha chuki eeeeh…
        Chuki yavunja umoja yeeeh..yooo…Kiberaaa!
        Kibera weee bwana Kiberaaa
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Oooo…yoooh Kiberaa
        Kiberaa wee bwana Kiberaaa
        Ooo… yeeeh Kiberaaa
        Kiberaa wacha wee Kiberaaa
        Oooo… yooo Kiberaaa
        Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
        Aaaa Ngulupaaa Ngulupaaa
        Aaaaa Ngulupaaa Ngulupaaaa
        Aaaa Ngulupaaa Ngulupaaa
        Ngulupaaa Ngulupaaa
        Ngulupaaa Ngulupaaaa
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibwacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Oooo…yoooh Kiberaa
        Kiberaa wee bwana Kiberaaa
        Ooo… yeeeh Kiberaaa
        Kiberaa wacha wee Kiberaaa
        Oooo… yooo Kiberaaa
        Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Oooo…yoooh
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Oooo…yoooh Kiberaa
        Kiberaa wee bwana Kiberaaa
        Ooo… yeeeh Kiberaaa
        Kiberaa wacha wee Kiberaaa
        Oooo… yooo Kiberaaa
        Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
        Kiberaa
        Kiberaa wee bwana Kiberaaa
        Ooo… yeeeh Kiberaaa
        Kiberaa wacha wee Kiberaaa
        Oooo… yooo Kiberaaa
        Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
        Ooooo..  yeee Kiberaa
        Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
        Oooo…yoooh Kiberaa
        Kiberaa wee bwana Kiberaaa
        Ooo… yeeeh Kiberaaa
        Kiberaa wacha wee Kiberaaa
        Oooo… yooo Kiberaaa
        Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa

        (IMEANDALIWA NA ALLY LITYAWI)
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: KIBERA ACHA CHUKI YA KASONGO MPINDA NA MK GROUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry