KIUNGO mtaalamu wa Mali, Seydou Keitaalitupia mopira nyavuni
zikiwa zimesalia dakika 10 na kuiwezesha Barcelona iliyokuwa pungufu ya
mchezaji mmoja kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Sporting Gijon katika La Liga
mwishoni mwa wiki.
Bao hilo liliifanya Barca inayoshika nafasi ya pili La Liga
iongoze kabla ya kupata linguine baadaye na kuwafanya mabingwa hao wa dunia, Ulaya
na Hispania sasa wawe wanazidiwa pointi 10 tu na vinara Real Madrid, zikiwa
zimebaki raundi 13 ligi kumaluizika.
Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Zidan alifunga bao lake la
tano Bundesliga, lakini halikuweza kuinusuru timu yajke, Mainz, kupigwa 2-1 na
vinara, Borussia Dortmund.
ENGLAND:
ALEX SONG (Arsenal)
Kiungo wa Cameroon, alitoa bonge la pasi kwa Robin van
Persie wakati The Gunners wakitoka nyuma na kuifunga Liverpool mabao 2-1 kwenye
Uwanja wa Anfield.
Pasi hiyo muruwa ya Song, alikutana nayo Van Persie dakika
ya mwisho na mshambuliajim huyo wa Kiholanzi akashangilia bao lake la 31 msimu
huu kwa kwenda kupiga busu kiatu cha Song.
STEVEN PIENAAR (Everton)
Kiungo wa Afrika Kusini alitoa pasi bab-kubwa kwa Royston
Drenthe wakati Everton ikitoka 1-1 na QPR. Pasi hiyo tamu ya Pienaar, iliunganishwa
kimiani na Drenthe dakika ya 31 na winga wa Kiholanzi Dutch akiwa umbali wa
mita 25.
DIDIER DROGBA (Chelsea)
Mshambuliaji wa Ivory Coast hakuwa na morali kabisa wakati Chelsea
inapigwa ‘kidude’ (1-0) na West Bromwich Albion katika mechi ya mwisho kwa
Andre Villas-Boas kuwa kocha wa Blues. Drogba alipata nafasi za kufunga na AVB akafukuzwa
ndani ya saa 24 baada ya kipigo hicho, ambacho kinawaacha Chelsea nafasi ya
tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
CHEICK TIOTE (Newcastle)
Kiungo wa Ivory Coast, alihusishwa na kadi nyekundu ya utata
aliyopewa kiungo wa Benin, Stephane Sessegnon katika sare ya 1-1 dhidi ya
Sunderland.
Sessegnon alimtoa njiani kwa bega Tiote dakika ya 58 ambalo lilikuwa
tukio la kawaida la kimchezo, lakini nyota huyo wa Newcastle alijiangusha ‘kiugizaji’
na kumfanya refa atoe kadi nyekundu.
MAHAMADOU DIARRA (Fulham)
Kiungo huyo wa Mali, aliichezea mechi ya kwanza Fulham na kutoa
pasi ya bao, wakati Cottagers wakiitandika Wolves mabao 5-0. Nyota huyo wa
zamani wa Real Madrid, Diarra, aliyejiunga na kikosi cha Martin Jol kama mchezaji
huru mwezi uliopita, baada ya kutemwa na Monaco, alitumia muda mwingi kuonyesha
uwezo wake baada ya kutokea benchi dakika ya 69 na pasi yake iliunganishwa vema
nyavuni na Clint Dempsey.
UFARANSA:
SIAKA TIENE (Paris Saint-Germain)
Tiene aliichezea mechi ya kwanza PSG tangu aiwakilishe Ivory
Coast kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika katika ushindi wa 4-1 dhidi
ya Ajaccio, ambao unaifanya timu ya Carlo Ancelotti kurejea kileleni mwa Ligi
Kuu.
Akichukua nafasi ya majeruhi Maxwell zikiwa zimesalia dakika
14, Tiene alisaidai kutengeneza bao la nne la PSG kwa kumimina krosi nzuri iliyounganishwa
kimiani na Clement Chantome.
AYMEN ABDENNOUR (Toulouse)
Beki wa kati wa Tunisia, Abdennour alifunga bao pekee na kuifanya
Toulouse kupata ushindi mzuri wa 1-0 dhidi ya Marseille, ambao unaipandisha
timu hiyo hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi. Abdennour alifunga dakika
ya 66, baada ya kwenda hewani zaidi ya Souleymane Diawara na kipa wa Marseille,
Steve Mandanda kuifuata kona iliyochongwa kutoka wingi ya kulia na Etienne
Didot na kuitumbukiza nyavuni kwa kichwa.
JONATHAN PITROIPA (Rennes)
Winga wa Burkina Faso, Pitroipa alikuwa nyota wa mchezo
wakati Rennes inawafunga wapinzan wao wa Brittany, Lorient mabao 2-0 na kupaa hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligue
1.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, alimalizia shambulizi
zuri la kushitukiza na kuwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 41, kisha
akamsetia mchezaji mwenzake wa Morocco, Youssouf Hadji kuifungia Rennes bao la
pili zikiwa zimesalia dakika 11.
UJERUMANI:
MOHAMED ZIDAN (Mainz 05)
Mshambuliaji wa Misri sasa amefunga katika mechi tano
mfululizo , lakini hakuweza kuiepusha timu yake na kipigo cha mabao 2-1 kutoka
kwa klabu yake ya zamani, Borussia Dortmund, ambayo aliachana nayo Januari tu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, aliisawazishia Mainz kwa
umahiri wa hali ya juu dakika ya 74, lakini Dortmund ikapiga la ushindi dakika
tatu baadaye, wakati Mjapan Shinji Kagawa alipotumbukiza nyavuni mpira.
MAME BIRAM DIOUF (Hanover 96)
Mshambuliaji wa Senegal, ambaye alijiunga na Hanover Januari
akitokea Manchester United, alifunga bao lake la pili katika mechi tano wakati
timu yake mpya ikitoka sare ya 2-2 na Augsburg.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipiga bao hilo kwa
kichwa dakika ya 69, kabla Augsburg kusawazisha kupitia kwa Jan-Ingwer
Callsen-Bracker kwa penalti dakika ya 89, baada ya kiungo wa Cameroon, Marcel
Ndjeng kuchezewa rafu.
ITALIA:
SULLEY MUNTARI (AC Milan)
Nyota wa AC Milan, ambaye alicheza vema mno katika sare ya
1-1 na Juventus wiki iliyopita, alipiga tena kazi nzuri katikam ushindi wa 4-0 dhidi
ya Palermo, akimsetia Zlatan Ibrahimovic bao lake la kwanza kati ya mtatu
aliyofunga dakika ya 21.
BOUKARY DRAME (Chievo)
Beki Msenegali aliyezaliwa Ufaransa, aliipa Chievo sare ya
1-1 na wawania ubingwa, Juventus,akifunga bao dakika ya 76, baada ya kazi nzuri
iliyofanywa na Davide Moscardelli.
HISPANIA
SOFIANE FEGHOULI (Valencia)
Mualgeria alifunga bao la ushindi, Valencia iking’ara
ugenini kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Granada, ambao unaiimarisha timu hiyo
katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Bao hilo lilikamilisha wiki nzuri kwa kiungo huyo, ambaye
alifunga bao la ushindi akiichezea kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa, dhidi
ya Gambia Jumatano.
FORMOSE MENDY (Sporting Gijon)
Winga wa Senegal, alicheza dakika zote kwa mara ya kwanza
katika klabu yake, Gijon ikipigwa mabao 3-1 na Barcelona kwenye Uwanja wa Camp
Nou.
Mendy, ambaye alianzia kazi Ufaransa, alifanya klazi nzuri
kwa kuitengenezea bao la kusawazisha Sporting kipindi cha pili, akitoa krosi
kwa Davd Barral aliyefunga.
SEYDOU KEITA (Barcelona)
Barcelona ilikuwa kwenye vita ya kung’oa pointi tatu, ikiwa
na wachezaji 10 tu uwanjani hadi guu la kushoto la kiungo wa Mali zikiwa zimesalia
dakika 10 lilipofanisha vita hiyo.
0 comments:
Post a Comment