Kikosi cha Yanga, ambacho leo jioni kitakuwa na kasheshe mbele ya Azam |
NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitawaka moto leo kwa mechi kali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara yenye mvuto wa michuano ya Afrika,
kama Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa.
Yanga
inashuka dimbani kumenyana na Azam, ikiwa ina
hasira nao ile mbaya Wana Lamba Lamba hao.
Hasira
za Yanga zinatokana na nini? Kwanza wamefungwa na Zamalek na kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mapema kama ilivyo kawaida yao.
Lakini
pili, Yanga imefungwa na Azam mara mbili mfululizo- kwanza kwenye mechi ya Ligi
Kuu 1-0 kwenye Ligi Kuu Septemba 18, mwaka jana Uwanja wa Taifa na baadaye kwenye
Kombe la Mapinduzi Januari, mwaka huu.
Lakini
yote tisa, 10 ni kwamba Yanga inataka kupoza machungu ya mashabiki wake baada
ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa- hivyo Jumamosi watataka kushinda kwa
lazima, licha ya ubora wa Azam wanaoutambua.
Yanga
iliyorejea Jumatatu kutoka Cairo, inasifiwa kucheza soka ya kuvutia licha ya kufungwa
na Zamalek, jambo ambalo linawafanya mashabiki wa timu hiyo wawe na hamu kubwa
ya kuiona timu yao.
Mechi
ya Jumamosi itawakutanisha vinara wa mabao katika Ligi Kuu, John Bocco kwa
upande wa Azam anayeongoza kwa mabao yake 12 na Kenneth Asamoah kwa Yanga,
anayefuatia kwa mabao yake 10.
Lakini
pia itawakutanisha makipa wanaowania kumvua glavu Juma Kaseja katika timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mwadini Ally wa Azam na Shaaban Kado wa Yanga
ambao wote ni makipa wa akiba katika kikosi cha Mdenmark Jan Borge Poulsen.
Haruna
Hakizimana Fadhil Niyonzima kwa sasa unaweza kusema ndiye mchezaji bora zaidi
wa kigeni katika Ligi Kuu- lakini Azam pia ina viungo wazuri wazawa kama Salum
Abubakar ‘Sure Boy’, Abdi Kassim ‘Babbi’ na Jabir Aziz, ambao wote wanaifanya
mechi hiyo iwe na ‘quality’ za Afrika.
Kocha
Muingereza Stewart Hall, baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu,
katika michuano iliyoshirikisha Simba na Yanga, tena akizifunga timu zote hizo,
ameweka bayana sasa anataka kufuta utawala wa vigogo hao na kwenye Ligi Kuu ya
Bara.
Lakini
kocha aliyekalia kuti kavu Yanga, Mserbia Kostadin Bozidar Papic hatahitaji
presha zaidi na dawa ya kuepuka hali hiyo ni ushindi tu Jumamosi.
Mambo
mengine yanayoifanya mechi hiyo iwe tamu ni kwamba Azam ina wachezaji ambao
misimu michache iliyopita walikuwa wanang’ara Yanga, kama Mrisho Ngassa na Abdi
Kassim.
Kocha wa Azam, Muingereza Steward Hall anaingia kwenye mchezo akiwa kumbukumbu ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union, wakati Mserbia wa Yanga, Kostadin Papic ana hasira za kipigo cha Cairo.
REKODI YA YANGA AZAM FC:
Septemba 18, 2011
Azam 1-0
Yanga
Machi 30, 2011
Yanga 2-1
Azam
Oktoba 24, 2010
Azam 0-0 Yanga
Machi 7, 2010
Yanga 2-1
Azam
Oktoba 17, 2009
Azam 1-1 Yanga
Aprili 8, 2009
Yanga 2-3
Azam FC
Oktoba 15, 2008
Azam FC 1-3
Yanga
0 comments:
Post a Comment