// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAPTENI STEVE AWAAMBIA VIJANA WAKAZE, HALI MBAYA NI AIBU KWA CHAMA KUBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAPTENI STEVE AWAAMBIA VIJANA WAKAZE, HALI MBAYA NI AIBU KWA CHAMA KUBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 13, 2012

    KAPTENI STEVE AWAAMBIA VIJANA WAKAZE, HALI MBAYA NI AIBU KWA CHAMA KUBWA


    Kapteni Steve
    NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard amewataka wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Anfield kujituma haswa baada ya kupokea kipigo cha tatu mfululizo kutoka kwa Sunderland Jumamosi.
    Wekundu hao hawajawahi kufungwa mechi tatu mfululizo tangu mwaka 2003, na kipigo hicho kinamuacha kocha Kenny Dalglish katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, pointi mbili tu dhidi ya wapinzani wao Everton watakaomenyana nao katika Merseyside derby Uwanja wa Anfield.
    "Wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa hapa tulipo kwenye ligi," alisema Gerrard said. Si nzuri kiasi cha kutosha kwa klabu kama yetu kuwa huko. Tunatakiwa kutafuta kiwango kizuri na cha kudumu. Tunahitaji kufanya kweli na hakuna timu nzuri ya kuifanyia hivyo zaidi ya Everton.
    Baada ya kutwaa Kombe la Ligi mwezi uliopita na kumaliza ukame wa mataji wa miaka sita, Liverpool imefufua matumaini ya kupigania Nne Bora katika Ligi ili icheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAPTENI STEVE AWAAMBIA VIJANA WAKAZE, HALI MBAYA NI AIBU KWA CHAMA KUBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top