// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAMATI YA TIBAIGANA YAMGWAYA RAGE, YAMPA ADHABU LAINIIIII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAMATI YA TIBAIGANA YAMGWAYA RAGE, YAMPA ADHABU LAINIIIII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 25, 2012

    KAMATI YA TIBAIGANA YAMGWAYA RAGE, YAMPA ADHABU LAINIIIII

    Tibaigana
    KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imempa onyo kali Mwenyekiti wa Simba SC, Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) kutokana na kauli za uchochezi anazodaiwa kutoa.
    Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Kamanda Mstaafu wa Kanda Maalum Jeshi la Polisi Dar es Salaam, imetoa onyo pia kwa Msemaji wa Yanga, Louis Sendeu kwa kosa kama hilo.
    Katika kikao chake cha jana kusikiliza tuhuma zilizowasilishwa na TFF, zilizohusisha matamshi yaliyotolewa na watuhumiwa hao kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga, Agosti 17, 2011.
    Katika mashitaka hayo, watuhumiwa hao walituhumiwa kukiuka Kanuni ya 30 (1) (f) na Kanuni ya 53 (1) (2) cha Kanuni za Adhabu za FIFA.
    Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kutafakari maelezo hayo, pamoja na kuchambua sheria na kanuni mbalimbali, Kamati imeamua yafuatayo:

    Hasara kwa Mdhamini
    Kuhusiana na suala hasara, Kamati inaona kwamba suala hili halikuwa na uzito wowote  wala hakukuwa na hoja ya msingi, wala ushahidi wa kuthibitisha kwamba tishio au matamko hayo yalikuwa na uhusiano na hasara inayodaiwa kwamba mdhamini huyo aliipata. Hakuna malalamiko yoyote yaliyotolewa kuhusiana na kinachodaiwa kuwa ni hasara inayotokana na matamko ya viongozi hawa. Kamati imeitupilia mbali hoja hii.

    Tuhuma za matamko ya watuhumiwa
    Kamati imebaini kwamba matamko hayo yalikuwa ni uvunjaji wa kanuni na yalilenga kuchochea hisia mbaya na kuleta vurugu. Kamati ina maoni ya kwamba viongozi wa vilabu hivi walistahili kufuata taratibu za kawaida katika kudai haki zao, badala ya kutoa matamko ambayo yangeweza kuchochea  hisia mbaya. Kitendo hicho si cha kiungwana na kinaendana kinyume na taratibu za uongozi wa mpira.
    Wao kama viongozi, walistahili kutumia utashi na kupima athari za matamko yao, ili kuepuka uwezekano wa kuleta msuguano usio wa lazima na kuungiza mchezo wa mpira katika kashfa au kukosa heshima. Matamko haya yanaweza kuwa ni kichocheo kwa viongozi wengine wenye tabia ya namna hiyo kutumia mwanya huu kufanya vitendo hivyo.
    Kwa msingi huo, Kamati inawaona wote wawili kuwa wana hatia na matamko hayo yanayohusiana na mchezo huo. Kwa kuzingatia hilo, Kamati inatoa onyo kali dhidi ya watuhumiwa hao wawili na inaonya kwamba adhabu kali zaidi zitachukuliwa kama watuhumiwa watalirudia kosa kama hili au linalofanana na hilo.
    Kamati imebaini pia kwamba Mheshimiwa Aden Rage amehusika pia na kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Bwana Saad Kawemba wa TFF, akidaiwa kwamba alikuwa anazuia usajili wa mchezaji Gervais Kago na kwamba Bwana Kawemba alifanya hivyo kwa vile ana mapenzi na klabu ya  pinzani ya Yanga.
    Pamoja na kwamba hakukuwa na athari za moja kwa moja dhidi ya Bwana Kawemba, ukweli ni kwamba kitendo hicho kilikuwa ni kosa ambalo halistahili kufanywa na kiongozi mwenye uzoefu mkubwa wa uongozi kama Mheshimiwa Rage, na kilikuwa kina dalili za kuchochea chuki zisizo na msingi dhidi ya Bwana Kawemba. Kitendo hicho kilikuwa kinakiuka kifungu cha 53 (1) (2) cha Kanuni za Adhabu za FIFA.
    Kamati inatoa onyo kali dhidi ya Mheshimiwa Aden Rage kwa kupatikana na hatia yake hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMATI YA TIBAIGANA YAMGWAYA RAGE, YAMPA ADHABU LAINIIIII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top