KIBIBI kizee cha Turin, Juventus jana kilizima gundu la
kucheza mechi nne bila ya kushinda, baada ya kuirarua 5-0 Fiorentina, ambayo
ilicheza zaidi ya saa moja na wachezaji 10.
Ikiwa bado haijafungwa msimu huu, Juve iko nafasi ya pili
ikiwa inazidiwa pointi nne na vinara AC Milan baada ya vinara hao kushinda 2-0 dhidi
ya Parma, mabao ya Zlatan Ibrahimovic kwa
penalti na Urby Emanuelson.
Milan, ambayo ilimuingiza uwanjani Gennaro Gattuso mwishoni
mwa mchezo kwa mara ya kwanza tangu apate matatizo ya macho Septemba, mwaka jana sasa ina pointi 60 kutokana
na mechi 28.
Mabao ya Jube yalifungwa na Mirko Vucinic dakika ya 5, Chilean
Arturo Vidal kabla ya mapumziko, Claudio Marchisio, Andrea Pirlo Simone Padoin walifunga
mabao mengine
0 comments:
Post a Comment